Kimataifa

Man City Yazima Dili la Barcelona kwa Dani Olmo

Man City Yazima Dili la Barcelona kwa Dani Olmo

Manchester City imewasilisha ofa kubwa kwa RB Leipzig kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na pia timu ya taifa ya Hispania, Dani Olmo, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha hili la usajili. Hatua hii inaweza kuvuruga mpango wa Barcelona wa kumleta staa huyo.

Olmo, mwenye miaka 26, anavutiwa na klabu nyingi za Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) na pia kwenye michuano ya Euro akiwa na timu ya taifa ya Hispania. Klabu ya kwanza kuripotiwa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili ilikuwa Barcelona, iliyoweka mezani Pauni milioni 40, lakini ofa hiyo ilikataliwa na Leipzig.

Mkataba wa sasa wa Olmo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayotaka huduma yake italipa Euro milioni 60.

Ingawa Olmo mwenyewe anaonekana kuwa na nia zaidi ya kujiunga na Barcelona badala ya Manchester City, kuingilia kwa Man City katika dili hilo kunaweza kumsababisha achague timu hiyo kutokana na ofa kubwa ambayo inadaiwa kuwekwa mezani.

Msimu uliopita akiwa na Leipzig, Olmo alicheza mechi 25 katika michuano yote, akafunga mabao manane na kutoa asisti tano. Katika michuano ya Euro akiwa na Hispania, alicheza mechi sita, akafunga mabao matatu na kutoa asisti mbili, na kuwa mmoja kati ya wachezaji waliopokea tuzo ya kiatu cha dhahabu.

Manchester City inataka kumsajili supastaa huyo kama sehemu ya maandalizi ya maisha bila kiungo wao nyota, Kevin de Bruyne, ambaye anahusishwa na timu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Leave a Comment