Matokeo ya Yanga Vs Red Arrows Leo Agosti 04, 2024 | Matokeo ya Mechi ya Kirafiki ya Yanga Day
Dar es Salaam, Agosti 4, 2024 – Leo ni siku ya kihistoria kwa klabu ya soka ya Yanga, maarufu kama “Young Africans,” wanapoadhimisha miaka 89 tangu kuasisiwa. Katika kilele cha sherehe hizi, Yanga wanachuana na mabingwa wa Kombe la Kagame 2024, Red Arrows ya Zambia, katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku.
Matokeo ya Yanga Vs Red Arrows Leo – Matokeo Yanga Day 2024
Yanga Sc | 2 – 1 | Red Arrows |
Kipindi cha Kwanza
- Mpira Umeanza Yanga 0 – 0 Red arrors
- Dakika ya 5 Yanga 0 – 1 Red arrors
- Mapumziko; Yanga 0 – 1 Red arrors
Kipindi cha Pili
- Kipindi cha Pili Yanga 0 – 1 Red arrors
- 64 Mudathir Anaipa Yanga 1 – 1 Red arrors
- 91 Aziz Ki Yanga 2 – 1 Red arrors kwa mkwaju wa penati
Tamasha la Yanga Day linafanyika siku moja tu baada ya Simba Day ambapo watani wao, Simba SC, walishinda 2-0 dhidi ya APR FC ya Rwanda. Wakati Simba wakisherehekea ushindi wao, Yanga nao wanajiandaa kwa tukio lao la kipekee.
Mashabiki na wadau wa soka wanatarajiwa kuujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa, wakisubiri kwa hamu kubwa mechi ya leo.
Katika mechi ya leo, Yanga inatambulisha kikosi chake kipya na jezi mpya kwa msimu wa 2024/2025. Mabingwa wa Kombe la Kagame 2024, Red Arrows ya Zambia, ni wapinzani wao wa leo. Hii ni nafasi kwa Yanga kuonyesha nguvu yao kabla ya msimu mpya kuanza.
Red Arrows ni timu yenye historia nzuri katika soka la Afrika Mashariki, na ushindani wao utaongeza hamasa katika mechi hii ya kirafiki. Mashabiki wanatarajia kuona mchezo mzuri na wenye ushindani mkali.
Mbali na mechi hii ya kirafiki, kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii maarufu ambao wataongeza shamrashamra za tamasha hili na kulipa radha na mvuto wa kipekee zaidi.
Tamasha la Yanga Day limekuwa ni sehemu muhimu ya utamaduni wa klabu hii, likiwakutanisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi.
Yanga inaingia kwenye mechi hii ikiwa na matumaini makubwa ya kuonyesha ubora wao na kutoa burudani kwa mashabiki wao. Mechi ya leo ni zaidi ya burudani; ni sehemu ya historia ya klabu hii kongwe.
Kwa mashabiki wa Yanga, leo ni siku ya kujivunia na kuonyesha mapenzi yao kwa timu yao pendwa kwa kutokea uwanjani na kulijaza dimba la Benjamin Mkapa kama walivyofanya mashabiki wa Simba.