Yanga Day 2024: Wiki ya Mwananchi ni sherehe kubwa inayofanyika leo kwa ajili ya Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara tatu mfululizo. Katika tukio hili la kipekee, mashabiki wa Yanga watasherehekea mafanikio ya timu yao kwa matukio ya kusisimua. Hizi hapa taarifa kuhusu bei za tiketi na tarehe ya tukio.
Yanga Day 2024 Tarehe na Mahali
Yanga Day 2024 inafanyika leo, tarehe 4 Agosti, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Sherehe hii hukutanisha mashabiki wa Yanga kwa burudani na utambulisho wa wachezaji wapya watakaowakilisha klabu katika msimu ujao.
Matukio ya Kutarajia Yanga Day 2024
Wiki ya Mwananchi itajumuisha matukio mbalimbali yenye lengo la kutoa burudani na kuimarisha mshikamano kati ya klabu na mashabiki wake. Baadhi ya matukio muhimu ni:
- Utambulisho wa Kikosi Kipya: Wachezaji wapya watawasilishwa mbele ya mashabiki kwa mara ya kwanza.
- Mechi ya Kirafiki: Yanga SC itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu nyingine, ikitumika kama majaribio ya mwisho kabla ya msimu rasmi kuanza.
- Burudani kutoka kwa Wasanii: Wasanii mbalimbali watatoa burudani ya muziki na ngoma.
- Hotuba na Sherehe: Viongozi wa klabu watazungumza na mashabiki kuhusu mipango na malengo ya msimu ujao.
Bei za Tiketi za Yanga Day 2024
Ili kuhakikisha kila shabiki anapata nafasi ya kushiriki katika sherehe hii, Yanga imeweka viwango tofauti vya tiketi:
- VIP A: Tsh 50,000
- VIP B: Tsh 30,000
- VIP C: Tsh 15,000
- Jukwaa la Machungwa: Tsh 10,000
- Mzunguko: Tsh 5,000
Tiketi za Royal
Pia, kutakuwa na tiketi za Royal zinazojumuisha jezi, siti za kukaa VIP A, huduma ya chakula, viburudisho, na usafiri kwa bei ya Tsh 300,000.
Wauzaji wa Tiketi za Yanga Day 2024
Tiketi za Yanga Day 2024 zinapatikana katika maeneo yafuatayo:
- Young Africans – Jangwani
- Vunja Bei – Kinondoni, Sinza, Mbeya
- T-Money Ltd – Kigamboni
- Gitano Samweli – Mbagala Zakiem
- Khalfan Mohamed – Ilala
- Kibacho Juma – Morogoro
- Mwanaidi Izina – Morogoro
- Godwin Fredy – Geita
- Twisty Investment – Geita
- Gwambina Lounge – Gwambina
- Karoshy Pamba – Dar Live (Zakhiem)
- Antonio Service – Sinza, Kivukoni
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign – Kinondoni Makaburini
- View Blue Skyline – Mikocheni
- Mkaluka Traders – Machinga Complex
- New Tech General Traders – Ubungo
- Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
- Juma Burrah – Mbeya, Kivukoni, Msimbazi
- Alphan Hinga – Ubungo
- Mtemba Service Co – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo
- Shirima Shop – Leaders
- Lampard Electronics – DSM