Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo, Agosti 24: Klabu Bingwa | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Vital’o CAF
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara, Klabu ya Yanga Sc leo itapambana na Vital’o ya Buruni katika mchezo wa marudiano wa michuano ya klabu Bingwa Afrika CAF katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi leo Agosti 24 majira ya saa moja usiku.
Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024
Yanga Sc | 1 – 0 | Vital’o |
Yanga, ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi ya kwanza ya michuano hii ya CAF Champions league 2024/2025 kwa kuwachapa Vital’o mabao 4-0, wanatazamiwa kuendeleza wimbi lao la ushindi mnene. Hata hivyo, kocha wao Miguel Gamondi ameonya kuwa bado hawajafuzu na wanapaswa kucheza kwa umakini mkubwa.
Mechi hii inatarajiwa kuwa yenye ushinani mkubwa kwani Vital’o watakuwa na kibarua kigumu cha kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza. Kocha wao, Parris Sahabo, amesisitiza kuwa hawatakwenda kujilinda bali watacheza kwa kushambulia ili kutafuta mabao.
- Klabu Bingwa Afrika CAF
- Young Africans SC VS Vital’O FC
- 24.08.2024
- Azam Complex
- Saa Moja Usiku
Matokeo ya Yanga dhidi ya Vitalo Leo
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, ameweka wazi kuwa ingawa walishinda kwa kishindo katika mchezo wa awali, hawachukulii mchezo wa leo kwa wepesi. Akisisitiza umuhimu wa tahadhari, Gamondi amesema kuwa wapinzani wao Vital’O wanaweza kuleta changamoto mpya, hivyo Yanga inatarajia kutumia kikosi chao kamili ili kupata ushindi na kufuzu kwa hatua inayofuata.
Tazama pia: Ugumu Wa Usajili Wa Khalid Aucho: Mavunde Afunguka
Yanga imejipanga vilivyo kuhakikisha wanapata matokeo bora zaidi, huku ikilenga kuandika historia mpya ya michuano ya CAF. Katika mchezo wa kwanza, walionyesha kiwango cha juu cha soka, wakimiliki mpira na kuonyesha ubora wa kiufundi. Ushindi wa leo utaipa Yanga fursa ya kujiandaa kwa hatua zinazofuata katika michuano hii ya kimataifa.
Leave a Comment