Yanga SC na Vital’o FC wanakutana leo katika hatua ya awali ya CAF. Pata matokeo na muonekano wa mechi hii muhimu.
Matokeo ya Yanga SC Vs Vital’o Leo 24/08/2024: Kuanza kwa Safari ya CAF Leo
Yanga | 1 – 0 | Vital’o |
Leo, tarehe 24/08/2024, Yanga SC wataanza rasmi safari yao ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kukutana na Vital’o FC ya Burundi. Mchezo huu utaanza saa kumi jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi. Inatarajiwa kuwa mechi hii itakuwa ya kuvutia na yenye ushindani mkali.
Soma pia: Kikosi Cha Yanga SC VS Vital’O Leo: Wachezaji Wanaoanza
Kocha Mkuu wa Vital’o FC, Sahabo Parris, amesema kwamba timu yake imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huu. Parris anaheshimu uwezo wa Yanga SC lakini anasisitiza kuwa mashindano haya ya Klabu Bingwa Afrika hayana mechi rahisi. Vital’o FC, yenye historia ya mafanikio nchini Burundi, ikiwemo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 1992, inajiandaa kwa matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri.
Kwa upande wa Yanga SC, Ofisa Habari wao, Ali Kamwe, amethibitisha kuwa timu iko tayari kutoa kiwango cha juu. Kamwe anasema kwamba Yanga SC inakwenda uwanjani kwa kujiamini licha ya changamoto kutoka kwa wapinzani wao. Wachezaji muhimu wa Yanga kama Clatous Chama, Aboutwalib Mshery, Djigui Diarra, Sure Boy, Aziz Ki, Farid Mussa, Maxi Nzengeli, na Pacome, wote wako fiti na wanatarajia kutoa burudani kubwa.
Mchezo huu ni wa kwanza kati ya miwili katika hatua ya awali ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Agosti 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Timu itakayoshinda jumla ya mechi hizi mbili itakutana na mshindi kati ya Commercial Bank of Ethiopia na Sports Club Villa ya Uganda katika raundi inayofuata.
Leave a Comment