Soka

Matumizi ya VAR Yaanza Rasmi Mechi ya Simba na Yanga

Matumizi ya VAR Yaanza Rasmi Mechi ya Simba na Yanga

Ni suala la muda kabla ya kujua iwapo ni hatua nzuri au kuna changamoto mbele yetu. Katika siku 11 zijazo, Simba na Yanga watakutana kwenye mechi ya Kariakoo Dabi katika Ngao ya Jamii, ambapo watapambana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2024-2025. Timu zote zimetoka katika matamasha yao, Simba Day na Wiki ya Mwananchi, katika uwanja huo huo.

Habari kutoka TFF zinaeleza kuwa teknolojia ya VAR inaweza kuanza kutumika katika mechi ya Kariakoo Dabi ya Ngao ya Jamii au mechi ya fainali ya michuano hiyo. Michuano hii inajumuisha timu nne: Azam, Coastal Union, Simba, na Yanga. Azam na Coastal Union zitakutana kwanza kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja Zanzibar, Agosti 8, na jioni yake Simba na Yanga watapambana uwanjani hapo.

Teknolojia ya VAR ilianza kutumika rasmi mwaka 2016 na Tanzania inajivunia kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kutumia teknolojia hiyo katika ligi yake. “Huenda VAR ikatumika katika mechi za Ngao ya Jamii kwa ajili ya majaribio kabla ya kuanza kutumika kwenye Ligi Kuu,” kilisema chanzo kutoka ndani ya TFF.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa wataalamu waliopewa mafunzo ya kutumia teknolojia hiyo, wakishirikiana na maofisa wengine, ndio watakaosimamia majaribio hayo. Hata hivyo, TFF inafanya siri kwa sasa.

Tangu taarifa kwamba VAR itaanza kutumika katika Ligi Kuu ya msimu ujao, wadau mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti. Wengine wanaamini itasaidia kupunguza dosari ambazo zimekuwa zikishusha hadhi ya ligi hiyo kwa misimu ya hivi karibuni, huku wengine wakiona inapaswa kutumika katika viwanja vyote, siyo kwa Mkapa tu.

Kuhusu ukweli wa suala hili, Mwenyekiti wa Mashindano wa TFF, Salum Madadi, alipendekeza kumtafuta Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko, Boniface Wambura, ingawa simu yake haikupokelewa.

Leave a Comment