Soka

Yanga Yatamba Tuzo za Ligi Kuu Bara, Simba Anapenya Mmoja Tu

Yanga Yatamba Tuzo za Ligi Kuu Bara

Yanga Yatamba Tuzo za Ligi Kuu Bara

Usiku wa tuzo za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 umefanyika jana katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, na matokeo yameonyesha nani amekuwa bora zaidi. Timu ya Yanga imeibuka kidedea kwa kutoa wachezaji 6 kwenye kikosi bora cha msimu wa 2023/24.

Kikosi hicho bora kinaongozwa na nyota wa Yanga, timu inayofundishwa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi. Kwa upande wa Simba, ambao ni wapinzani wao wa jadi, ni mchezaji mmoja tu aliyeingia kwenye kikosi cha kwanza.

Kikosi bora cha msimu ni kama ifuatavyo:

  • Golikipa: Ley Matampi wa Coastal Union
  • Beki wa Kulia: Yao Kouassi wa Yanga
  • Beki wa Kushoto: Mohamed Hussen wa Simba
  • Beki wa Kati: Ibrahim Hamad wa Yanga
  • Beki wa Kati: Dickson Job wa Yanga
  • Kiungo: Mudathir Yahya wa Yanga
  • Kiungo: Kipre Junior wa Azam FC
  • Kiungo: Maxi Nzengeli wa Yanga
  • Winga: Wazir Junior wa KMC
  • Winga: Feisal Salum wa Azam FC
  • Mshambuliaji: Aziz Ki wa Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephanie Aziz Ki, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2023/24. Aziz Ki ameshinda tuzo nne muhimu ambazo ni mchezaji bora (MVP), kiungo bora wa Ligi Kuu, mfungaji bora wa Ligi Kuu, na tuzo ya kikosi bora cha msimu. Amefanikiwa kuwashinda Kipre Junior wa Azam FC na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC katika tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu msimu wa 2023/24.

Leave a Comment