Soka

Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025

Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025

Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025 | Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi majina ya wachezaji watakaojiunga na kambi ya maandalizi ya Timu ya Taifa Stars kwa ajili ya michezo miwili muhimu ya kufuzu kwa michuano ya Afrika Cup of Nations (AFCON) 2025. Timu ya Taifa Stars inatarajiwa kucheza dhidi ya Ethiopia na Guinea katika juhudi za kupata nafasi ya kushiriki kwenye fainali za AFCON 2025.

Kocha Hemed Suleiman ameita kikosi kinachojumuisha wachezaji wanaofanya vizuri kutoka vilabu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Wachezaji hao wamechaguliwa kwa umakini mkubwa kulingano na uwezo wao wa kulisakata kabumbu ili kuhakikisha kuwa Taifa Stars inakuwa na kikosi imara na kinachoweza kukabiliana na ushindani mkali wa kimataifa.

Wachezaji Walioitwa Timu ya Taifa Kufuzu Afcon 2025

  1. Ally Salim – Simba SC
  2. Abdultwalib Mshery – Young Africans
  3. Yona Amos – Pamba SC
  4. Lusajo Mwaikenda – Azam FC
  5. Nathaniel Chilambo – Azam FC
  6. Mohamed Hussein – Simba SC
  7. Dickson Job – Young Africans
  8. Pascal Msindo – Azam FC
  9. Ibrahim Hamad – Young Africans
  10. Bakari Nondo – Young Africans
  11. Nickson Kibabage – Young Africans
  12. Abdulmalik Zakaria – Mashujaa FC
  13. Adolf Mtasigwa – Azam FC
  14. Himid Mao – Tala’a El Geish, Misri
  15. Novatus Dismas – Goztepe, Uturuki
  16. Mudathir Yahya – Young Africans
  17. Hussein Semfuko – Coastal Union
  18. Edwin Balua – Simba SC
  19. Feisal Salim – Azam FC
  20. Wazir Junior – Dodoma Jiji
  21. Cyprian Kachwele – Vancouver Whitecaps, Canada
  22. Clement Mzize – Young Africans
  23. Abel Josiah – TDS TFF Academy

Leave a Comment