Soka

Moses Phiri Ajiunga na Power Dynamos

Moses Phiri Ajiunga na Power Dynamos

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Moses Phiri, amejiunga na Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuhitimisha mkataba wake na Simba.

Moses Phiri Ajiunga na Power Dynamos kwa Mkataba wa Miaka Miwili

Mshambuliaji huyo alijiunga na timu hiyo kwa mkopo mnamo Januari 16, mwaka huu akitokea Simba SC, baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza na kuamua kutafuta changamoto mpya.

Moses Phiri Ajiunga na Power Dynamos kwa Mkataba wa Miaka Miwili
Moses Phiri Ajiunga na Power Dynamos kwa Mkataba wa Miaka Miwili

Phiri, ambaye alijiunga na Simba SC mnamo Juni 15, 2022, alimaliza mkataba wa miaka miwili aliosaini wakati anahama kutoka Zanaco. Hata hivyo, kulikuwa na kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi, lakini hakukitumia.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Zambia, Phiri alieleza kuwa amekuwa na mazungumzo na timu kadhaa na ataweka wazi uamuzi wake hivi karibuni kuhusu atakapoelekea msimu ujao, huku akiwataka mashabiki waendelee kumpa sapoti.

“Timu nyingi zimeonyesha nia ya kuhitaji saini yangu, lakini bado sijafanya uamuzi wa mwisho wa wapi nitacheza msimu ujao. Suala hilo kwa sasa nimewaachia wawakilishi wangu walifanyie kazi na litakapokamilika nitaliongelea,” amesema.

Wakati akitoa maelezo hayo, mmoja wa marafiki zake wa karibu, ambaye hakutaka kutajwa jina, aliliambia Mwanaspoti kwamba Phiri ameshasaini mkataba wa kuichezea Power Dynamos na tayari ameanza maandalizi ya msimu mpya na kikosi hicho.

“Dynamos imetoka makao makuu yake mjini Kitwe na imeelekea mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu. Phiri ni mmoja wa nyota wapya waliosajiliwa,” alisema rafiki huyo.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa Simba SC, Phiri alikuwa na mafanikio makubwa akifunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara, akiwa nyuma ya vinara Fiston Mayele wa Yanga na Said Ntibazonkiza ‘Saido’ wa Simba, ambao kila mmoja alifunga mabao 17.

Hadi anaondoka Simba Januari mwaka huu kurudi Zambia, Phiri alikuwa amefunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara. Wakati alipojiunga na Simba SC mnamo Juni 15, 2022, alitoka kushika nafasi ya pili kwa mabao mengi kwenye Ligi Kuu Zambia akiwa na Zanaco, ambapo alifunga mabao 14, nyuma ya Ricky Banda wa Red Arrows aliyefunga mabao 16.

Leave a Comment