Soka

Joshua Mutale asifiwa na Saleh Jembe

Joshua Mutale asifiwa na Saleh Jembe

Mchambuzi maarufu wa michezo, Saleh Jembe, ni miongoni mwa wale waliohudhuria kambi ya mazoezi ya Simba nchini Misri, wakijiandaa kwa msimu wa Ligi Kuu Bara 2024/25. Akiandika kuhusu winga wa Simba, Joshua Mutale, Saleh Ally alieleza:

Kisukuma Mutale ina maana ya ‘mkubwa’, lakini anahitaji kidogo kuvuta neno hilo… Huyu Mutale wa Simba kwa kiumbo si mkubwa sana, lakini uwezo wake ni mkubwa na ataibua gumzo.

Joshua Mutale ana kasi, nguvu, na si mwoga. Ana uwezo wa kuwatambuka walinzi hadi watatu kwa wakati mmoja. Hasa ni hatari zaidi anapopiga mashuti yake makali. Mfano mzuri ni bao la pili la Simba dhidi ya Wasaudi, ambapo alipokea mpira pembeni, akasonga kwa kasi na kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi ndani.

Wakati walinzi walijaribu kujipanga dhidi ya kasi yake, Mutale alifika tena na kupiga shuti lingine, bao la uhakika. Kwa hakika, Joshua Mutale ni miongoni mwa usajili bora wa Simba na anatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya timu hiyo msimu huu.

Leave a Comment