Simba SC

Willy Onana Kuondoka Simba

Willy Onana Kuondoka Simba

UJIO wa kipa mpya kutoka Guinea, Moussa Camara ‘Spider’ umemfanya winga wa Simba, Willy Onana kung’oka Msimbazi baada ya taarifa kuvunja ni yeye ndiye anayempisha kipa huyo aliyetua kuziba nafasi ya Ayoub Lakred aliyeumia kambini Misri.

Taarifa ambazo Mwanaspoti tangu awali ilishazidokeza katika matoleo ya nyuma kwamba, kipa huyo aliyepewa mkataba wa miaka miwili akitua tu Msimbazi, basi Mcameroon huyo atachomolewa kikosini zimedhihiri.

Usajili wa Camara ni wa dharura kutokana na kuumia kwa Ayoub Lekred, ambaye alionekana tegemeo ndani ya kikosi hicho, hivyo ujio wake utaongeza nguvu dhidi ya makipa wenzake Hussein Abel na Ally Salim.

Willy Essomba Onana Qatar

Katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo, yaliofanyika leo Ijumaa Agosti 3, 2024, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Onana hakuwa sehemu ya kikosi na taarifa za ndani zinaeleza keshapata timu huko Qatar anayoweza kujiunga nayo wakati wowote.

Mwanaspoti lilikuwa la kwanza kuripoti taarifa za endapo kama dili la Camara likiti Onana atakatwa na ndicho kilichotokea.

“Onana hatakuwa sehemu ya timu kwa msimu ujao, tumefanya hivyo ili kusalia na wachezaji 12 wa kigeni, bahati nzuri alikuwa analijua hilo tangu tupo Misri kwenye maandalizi ya msimu mpya,” amesema kiongozi mmoja wa timu hiyo.

Simba ilimsajili Onana msimu uliopita kutoka Rayon Sports ya Rwanda akiwa mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo (MVP).

Leave a Comment