Yanga SC

Yanga Yatua Dar Baada ya Ushindi vs Kaizer Chiefs

Yanga Yatua Dar Baada ya Ushindi vs Kaizer Chiefs

Yanga Yatua Dar Baada ya Ushindi Mkubwa

Mabingwa wapya wa Kombe la Toyota 2024, Yanga, wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho, Julai 30, 2024, wakitokea Afrika Kusini.

Yanga wanarejea nyumbani kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs, na hivyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Toyota kwa mwaka huu wa 2024.

Mabao hayo muhimu yaliyoipa Yanga ushindi yalifungwa na wachezaji mahiri Prince Dube, Clement Mzize, na Stephane Aziz Ki aliyetikisa nyavu mara mbili.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha Nasreddine Nabi tangu aliporejea kuinoa timu, lakini alipata kichapo kutoka kwa timu yake ya zamani.

Kikosi cha Wananchi kinawasili Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na Wiki ya Mwananchi, ambayo itahitimishwa Agosti 4, 2024, kwa mechi kali dhidi ya Red Arrows.

Leave a Comment