Yanga SC

Kikosi Cha Yanga SC VS Vital’O Leo: Wachezaji Wanaoanza

Kikosi Cha Yanga SC VS Vital’O Leo: Wachezaji Wanaoanza

Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo 17/08/2024 CAF Champions League, Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi ya Vital’o Klabu Bingwa Afrika.

Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo
Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo

Leo, 17 Agosti 2024, Yanga SC itachuana na Vital’O FC kutoka Burundi katika michuano ya CAF Champions League. Mchezo huu utaanza majira ya saa kumi jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi. Michuano hii ni hatua muhimu kwa Yanga SC, kwani inasherehekea mwanzo mpya katika safari yao ya kimataifa.

Kikosi Cha Yanga SC VS Vital’O Leo 17/08/2024

Hiki hapa ndicho kikosi rasmi cha Yanga leo

  • 59 Diarra
  • 21 Yad
  • 30 Kibabage
  • Mwamnyeto
  • 4 Bagga
  • Augho
  • Maxi
  • Mudathir
  • 24 Dube
  • 10 A212 Ki
  • 12 Chama

Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania na Ngao ya Jamii, wanaingia uwanjani wakiwa na hali nzuri baada ya ushindi mkubwa wa 4-1 dhidi ya Azam FC. Kocha wao, Miguel Gamondi, amesisitiza umuhimu wa nidhamu ya kiufundi na umakini mkubwa kutoka kwa wachezaji wake katika mchezo huu wa kwanza. Gamondi anatamani kushinda mchezo huu ili kuweka mazingira mazuri kwa mchezo wa marudiano.

Kocha wa Vital’O FC, Sahabo Parris, amekiri kuwa anaheshimu Yanga SC kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, lakini ameonya kuwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika haileti mechi rahisi. Vital’O FC, timu yenye historia kubwa nchini Burundi, ilishinda mataji 21 ya Ligi Kuu na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 1992. Msimu huu, walimaliza kama mabingwa wa Ligi Kuu ya Burundi, wakiwa na alama 72 katika michezo 30.

Kwa upande wa Yanga SC, wachezaji kama Clatous Chama, Jean Baleke, na Farid Mussa wanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa. Aidha, wachezaji wapya Duke Abuya na Prince Dube wameonyesha kiwango bora tangu walipojiunga na timu hiyo, hivyo kuongeza matumaini ya Yanga SC kufanya vizuri katika michuano hii.

Matokeo ya Klabu Bingwa leo

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC, ametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi na kuwapa sapoti wachezaji. “Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi na kutupatia sapoti, kwani hakuna mchezo rahisi katika Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Kamwe.

Taarifa kamili kuhusu kikosi cha Yanga SC VS Vital’O, kitakachoitwa na kocha mkuu wa Yanga lisaa limoja kabla ya mchezo, itatolewa hivi karibuni.

Leave a Comment