Jinsi Ya

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (Jinsi ya kujua salio NSSF)

Neno NSSF limetokana na maneno ya kingereza “National Social Security Fund” ambayo kwa kiswahili ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii. NSSF ni taasisi ya serikali ya Tanzania inayohusika na ukusanyaji, uwekezaji, na usambazaji wa michango ya wafanyakazi ili kuhakikisha maisha bora baada ya kustaafu. Ni muhimu kwa kila mfanyakazi kufahamu salio lake ili kupanga mustakabali wake kifedha.

Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (Jinsi ya kujua salio NSSF)

Kwa wale wanaotaka kuangalia salio lao la NSSF kwa kutumia simu, kuna njia rahisi na ya haraka ya kufanya hivyo. Unachohitaji ni kuwa na simu yako yenye mtandao wa Tigo au Vodacom, na kufuata hatua zifuatazo:

Kuangalia Salio La NSSF Kwa Njia Ya SMS

  1. Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
  2. Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Balance” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Balance 123456789.
  3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.

Kupata Taarifa ya Statement ya Akaunti ya NSSF Kwa Njia Ya SMS

  1. Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
  2. Tuma ujumbe wenye neno “NSSF Statement” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama wa NSSF. Mfano: NSSF Statement 123456789.
  3. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.

Kuangalia Salio La NSSF WhatsApp

  1. Hifadhi namba 0756 140 140 kwenye simu yako.
  2. Fungua WhatsApp na tuma ujumbe “Hello” au “Habari”.
  3. Fuata maelekezo ili kuangalia salio lako (“Balance”) au taarifa za michango (“Statement”)

Jinsi ya Kuangalia Salio la NSSF kwa Programu ya Simu Janja

  1. Pakua programu ya “NSSF Taarifa” kutoka Google Play Store.
  2. Ingia kwa kutumia maelezo yako ya NSSF.
  3. Angalia salio lako, michango, na taarifa nyingine muhimu.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

  • Salio unalopokea kwa njia ya simu linaweza kuwa tofauti kidogo na lile utakalopewa moja kwa moja kwenye ofisi za NSSF. Hii ni kwa sababu kunaweza kuwa na mabadiliko madogo ambayo hayajaingizwa kwenye mfumo wa simu bado.
  • Njia Nyingine: Ili kupata taarifa kamili na sahihi zaidi, tembelea ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe.
Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)
Jinsi Ya Kuangalia Salio NSSF Kwa Simu (NSSF Balance Check)

Mawasiliano Zaidi na NSSF

Ikiwa unahitaji maelezo zaidi au msaada, unaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa NSSF kwa kutumia mawasiliano yafuatayo:

  • Barua pepe: [email protected]
  • Simu: 0 (75) 6140140 | 0800116773 | (255) (22) 2200037
  • Anwani: National Social Security Fund, P.O.Box 1322, Benjamin Mkapa Pension Towers, Azikiwe St, Dar Es Salaam, Tanzania.

Leave a Comment