Kikosi cha Simba SC kinachoenda South kuikabili Stellenbosch

0
Kikosi cha Simba SC kinachoenda South kuikabili Stellenbosch

Kikosi Rasmi Simba SC Kitakachoikabili Stellenbosch Nusu Fainali ya Pili CAF Confederation Cup

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kikosi cha wachezaji 23 watakaosafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Pili ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup) msimu wa 2024/2025 dhidi ya Stellenbosch FC. Safari hiyo inatarajiwa kuanza Jumatano tarehe 23 Aprili 2025, asubuhi kupitia Shirika la Ndege la Air Tanzania kutoka Dar es Salaam hadi Johannesburg, kisha kuelekea mji wa Durban.

Mchezo huo muhimu utafanyika tarehe 27 Aprili 2025 kwenye Uwanja wa Moses Mabhida kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Simba SC inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Matokeo ya ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo huu wa marudiano yataihakikishia Simba kufuzu kwa mara ya kwanza kwenye Fainali ya CAF Confederation Cup.

Kikosi cha Simba SC Kitakachoikabili Stellenbosch Nusu Fainali ya Pili

Hiki hapa ni kikosi kamili cha wachezaji wa Simba SC watakaokabiliana na Stellenbosch:

Makipa

Na.Jina
1Moussa Camara
2Hussein Abel
3Ally Salim

Mabeki

Na.Jina
4Chamou Karaboue
5Mohamed Hussein
6Shomari Kapombe
7Abdurazack Hamza
8David Kameta
9Che Fondoh Malone
10Valentino Nouma

Viungo

Na.Jina
11Joshua Mutale
12Augustine Okejepha
13Jean Charles Ahoua
14Fabrice Ngoma
15Awesu Awesu
16Yusuph Kagoma
17Kibu Denis
18Debora Fernandes
19Ladack Chasambi
20Edwin Balua
21Elie Mpanzu

Washambuliaji

Na.Jina
22Steven Mkwala
23Leonel Ateba

Simba SC sasa inaelekea kwenye moja ya mechi zake muhimu zaidi katika historia ya mashindano ya CAF, ikisaka tiketi ya kuandika historia mpya kwa kushiriki fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here