KenGold Yashuka Daraja Rasmi, Yasaka Heshima Mechi Zilizobaki

0
KenGold Yashuka Daraja Rasmi, Yasaka Heshima Mechi Zilizobaki
KenGold Yashuka Daraja Rasmi, Yasaka Heshima Mechi Zilizobaki

KenGold Yathibitisha Kushuka Daraja Mapema Kabla ya Msimu Kumalizika

Timu ya KenGold imeshuka daraja rasmi kabla ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025, baada ya kucheza mechi 27 na kujikusanyia pointi 16 pekee. Hata kama watashinda mechi zao tatu zilizobaki, bado hawawezi kufikia pointi za timu iliyo katika nafasi ya 14 ambayo ndiyo ya mwisho kwa kuepuka kushuka daraja au kwenda kwenye hatua ya mtoano.

Mechi Zilizobaki kwa KenGold

Kwa sasa, KenGold inakabiliwa na mechi tatu za kumalizia ratiba, lakini matarajio ya kupata alama katika mechi hizo ni madogo kutokana na changamoto za wapinzani waliopo mbele yao.

Pamba FC vs KenGold

Katika mechi dhidi ya Pamba, ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa. Pamba nao wanapambana kuepuka kushuka daraja, hivyo wataingia uwanjani kwa lengo la kupata pointi zote tatu. Hii itakuwa kazi ngumu kwa KenGold kupata matokeo chanya kwenye uwanja huu mgumu.

KenGold vs Simba SC

Mechi dhidi ya Simba SC ni moja ya ngumu zaidi. Simba bado ipo kwenye mbio za ubingwa na kila mchezo kwao ni muhimu. Hivyo, matarajio ya KenGold kupata alama yoyote ni finyu mno, hasa kutokana na tofauti kubwa ya ubora kati ya timu hizo.

Namungo FC vs KenGold (Ugenini Lindi)

Mchezo wa mwisho wa KenGold utakua dhidi ya Namungo FC mjini Lindi. Namungo pia huenda wakawa bado wanahitaji pointi kwa ajili ya kutimiza malengo yao msimu huu, hivyo wataingia na ari ya ushindi. Kwa KenGold, hii itakuwa mechi ya kutafuta heshima pekee.

Matokeo na Hatima ya KenGold

Katika mechi hizi tatu, KenGold ina nafasi ndogo ya kupata ushindi. Kwa mujibu wa tathmini ya kiufundi, kikosi hiki kitaweza kuongeza sare moja tu, hivyo kumaliza msimu kwa jumla ya pointi 17. Msimu huu umekuwa wa changamoto kubwa kwao, na sasa wanarejea kwenye Ligi ya Championship (Ubingwa) wakiwa na matumaini ya kujipanga upya kwa msimu ujao.

KenGold itahitaji kufanya maboresho makubwa ili kurudi tena Ligi Kuu wakiwa na nguvu na ushindani zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here