Yanga na Azam FC wanakutana tena kwenye fainali ya Ngao ya Jamii 2024/25. Je, nani ataibuka mshindi? Angalia rekodi zao za awali!
Yanga na Azam FC Katika Vita ya Ngao ya Jamii
Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, watakutana tena na Azam FC, maarufu kama Waoka Mikate wa Chamazi, katika fainali nyingine muhimu ya Ngao ya Jamii kwa msimu wa 2024/25. Timu hizi zimekuwa zikikumbana mara kwa mara kwenye fainali za hivi karibuni, na huu ukiwa ni mkutano wao wa tatu mfululizo.
Katika mechi ya hivi karibuni, Yanga iliifunga Simba SC kwa bao 1-0 na kutinga fainali, ambapo Maxi Mpia Nzengeli alifunga bao hilo akipokea pasi safi kutoka kwa Prince Dube. Mchezo huu unakuja baada ya Yanga na Azam FC kukutana kwenye fainali mbili za awali, ikiwemo:
- Yanga 1 – 0 Azam (FA)
- Yanga 0 – 0 Azam (FA), Yanga ikishinda 7-6 kwa mikwaju ya penalti
Kwa upande mwingine, Azam FC imekuwa ikipambana vikali dhidi ya Coastal Union katika hatua za nusu fainali za mashindano mbalimbali:
- 21/22: Azam ilipoteza dhidi ya Coastal Union kwenye nusu fainali (FA), na Yanga ilishinda ubingwa kwa kuifunga Coastal Union kwenye fainali.
- 22/23: Azam ilishinda dhidi ya Coastal Union kwenye nusu fainali (FA) na kukutana na Yanga kwenye fainali, ambapo Yanga ilitwaa ubingwa.
- 23/24: Azam ilishinda dhidi ya Coastal Union katika nusu fainali ya Ngao, na sasa itakutana na Yanga katika fainali.
Ushindani kati ya Yanga SC na Azam FC umeleta mvuto mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini, huku rekodi zikionyesha namna timu hizi zinavyopambana kwa kila nafasi.
Leave a Comment