Michezo

Wydad Casablanca Yapania Kumsajili Mzize kwa Bilioni 2.1

Wydad Casablanca Yapania Kumsajili Mzize

Wydad Casablanca yatuma ofa ya Bil 2.1 kwa Yanga kumsajili Clement Mzize, pamoja na pre-season Morocco. Je, Yanga itakubali?

Wydad Casablanca Yaimarisha Ofa kwa Clement Mzize

Klabu ya Wydad Casablanca kutoka Morocco imetuma ofa ya tatu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, baada ya kuongeza dau la usajili kufikia takribani Tsh Bilioni 1.4. Ofa hiyo inaweza kufikia hadi Tsh Bilioni 2.1 kutegemea na makubaliano ya ziada kati ya klabu hizo mbili.

Ofa ya Pre-season na Usajili wa Kipekee

Mbali na dau la pesa, Wydad pia imeipa Yanga ofa ya kuandaa kambi ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season) nchini Morocco. Katika ofa hiyo, Wydad itagharamia kila kitu kwa Yanga, ikiwemo malazi, mazoezi, na vifaa vingine vya timu.

Ushawishi wa Kocha Rulani Mokoena

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Morocco, Wydad Casablanca inaamini kuwa ofa hii ni kubwa na ya kuvutia, na kwamba Yanga inaweza kumruhusu Mzize kujiunga na timu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na kocha Rulani Mokoena, aliyewahi kufundisha Mamelodi Sundowns. Uwezo na umahiri wa Mokoena unatabiriwa kumsaidia Mzize kung’ara zaidi.

Yanga Yasimama Kidete na Msimamo Wake

Hata hivyo, Yanga bado imesisitiza kuwa haitamuuza Mzize chini ya dau lisilopungua Tsh Bilioni 2.7. Msimamo huo unaashiria kuwa klabu hiyo inamtambua vyema thamani ya mchezaji huyo na haitakubali kushusha kiwango cha fedha wanachokihitaji.


Kwa kuwa Wydad inaonekana kuwa na nia ya dhati ya kumsajili Mzize, itabakia kuona kama Yanga itapunguza msimamo wake au itakubali dau hilo kubwa lililowekwa mezani na matajiri hao wa Morocco.

Leave a Comment