Audio

Wasanii Maarufu Waliohama Kati ya Simba na Yanga

Wasanii Waliohama Kati ya Simba na Yanga

WASANII WALIOHAMA KATI YA SIMBA NA YANGA

Katika ulimwengu wa soka, wasanii maarufu hapa Tanzania wamekuwa wakihama kutoka timu moja kwenda nyingine, wakileta msisimko kwa mashabiki wao. Msimu huu na uliopita, tumeona wasanii wakibadilisha timu zao kati ya Simba na Yanga. Hapa chini ni orodha ya baadhi ya wasanii hao:

Ali Kiba

Supastaa wa Bongo Fleva na mwanasoka, Ali Kiba, aliyejulikana kama shabiki wa Yanga, amehamia Simba na kutumbuiza kwenye Simba Day tangu msimu uliopita.

Diamond Platnumz

Nyota wa Bongo Fleva, Diamond, ambaye awali alikuwa shabiki wa Simba, sasa amehamia Yanga. Alieleza kuwa Haji Manara ndiye aliyemshawishi kujiunga na Yanga.

Harmonize

Msanii mwingine maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize, ambaye alikuwa shabiki wa Simba, amehama na kujiunga na Yanga. Alitumbuiza kwenye Wiki ya Mwananchi na kuendelea kuonyesha upendo wake kwa Yanga.

Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo Muvi, Shamsa Ford, aliyekuwa shabiki wa Simba, sasa ni shabiki wa Yanga.

Irene Uwoya

Muigizaji wa Bongo Muvi, Irene Uwoya, anayejulikana kama shabiki wa Yanga, hivi karibuni alionekana akiwa amevalia jezi ya Simba. Amesema ilikuwa ni kazi tu, lakini wapo wanaodai amehamia Simba.

Marioo

Msanii wa kizazi kipya, Marioo, ambaye awali alikuwa shabiki wa Simba, sasa ni shabiki wa Yanga. Ameeleza kuwa hama kwa sababu Simba ilikuwa ikimsababishia msongo wa mawazo.

Paula

Paula, mtoto wa msanii wa filamu Kajala Masanja, ambaye awali alikuwa shabiki wa Simba, sasa amejiunga na Yanga kumfuata mzazi mwenzie, Marioo.

Meja Kunta

Msanii maarufu wa Singeli, aliyejulikana kwa kibao chake cha “Mamu,” awali alikuwa shabiki wa Simba. Hata hivyo, msimu huu amehama na kujiunga na Yanga, akipewa nafasi ya kutumbuiza siku ya Wananchi.

Chino

Mwimbaji wa Bongo Fleva, Chino, aliyekuwa akiishabikia Yanga, msimu huu alihamia Simba na kutumbuiza kwenye Simba Day. Aliungana na wakali kama AliKiba na Joh Makini kwenye sherehe hizo.

Rushayna

Mrembo na muigizaji wa tamthilia, ambaye awali alikuwa shabiki wa Yanga, sasa amejiunga na Simba. Alionekana kwenye Simba Day akiwa amevalia jezi za Msimbazi.

Husna Sajenti

Msanii wa Bongo Muvi, Husna Sajenti, amekuwa akihama kati ya Simba na Yanga mara kadhaa. Kwa sasa amejiunga na Yanga.

Wasanii hawa wameleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania kwa maamuzi yao ya kubadilisha timu. Ni wazi kuwa soka lina nafasi kubwa katika maisha yao na wanatumia ushawishi wao kuburudisha na kuwafurahisha mashabiki wao.

Leave a Comment