Urusi imeahidi kuendelea kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Afrika, ili kuchochea Maendeleo kupitia miradi mbalimbali kupitia ushirikiano wa vyombo vya habari.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa pamoja uliofanyika
Duma ya Jimbo la Shirikisho la Urusi mnamo Machi 6, 2025 ukihusisha wadau mbalimbali kama wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, waandishi wa habari wakuu, wahariri, wanablogu maarufu, na wataalamu wa usalama wa habari.
Tukio hilo liliongozwa na Baraza la wataalam wa Maendeleo na Usaidizi wa Ushirikiano wa kina na Nchi za Afrika, likiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Duma ya Jimbo la Shirikisho la Urusi, A. Babakov, na Chama cha Nishati cha Afrika-Urusi.

Ushirikiano huu unatarajia kuboresha mtandao wa habari na kuimarisha ushirikiano wa pande zote mbili kupitia majadiliano ya kina kuhusu changamoto na fursa zilizopo kati ya pande zote mbili.
Wadau na wataalamu wa sekta ya habari walipata nafasi ya kuchangia mawazo na mapendekezo kuhusu matumizi bora ya vyombo vya habari na mitandao (Blog) ili kuendeleza miradi ya pamoja na kuongeza ushirikiano katika sekta ya mawasiliano.
Alexander Babakov alifungua tukio kwa kusisitiza kwamba matatizo ya mawasiliano kati ya Urusi na Afrika hayatatatuliwa bila ushiriki wa serikali akihimiza kuhakikisha ushawishi wa serikali na kuunda mazingira yatakayosaidia utekelezaji wa ajenda yetu ya habari kwa kuleta sera za kitaifa zinazoweza kuimarisha uhusiano wa vyombo vya habari.
Kwa upande wake Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova, amebainisha kuwa ni muhimu kuendeleza mawasiliano kupitia programu za kielimu, ziara za waandishi wa habari, na mikutano mikubwa ili kuhakikisha hadhira ya Afrika inapokea taarifa sahihi na za kina kuhusu uhusiano huu.

Elimu na ushirikiano katika sekta ya vyombo vya habari ulianzishwa kutokana na maoni kutoka kwa watendaji kama Clarissa Vaidorven na Svyatoslav Shchegolev ambao waliona umuhimu wa kuimarisha uhusiano huo.
Leave a Comment