Vituo vya Kununua Tiketi Mechi ya Simba SC vs Stellenbosch FC – 20/04/2025
Simba SC kutoka Tanzania itacheza na Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini kwenye mechi ya nusu fainali ya CAF Confederation Cup. Mchezo huu wa kusisimua utachezwa Jumapili, tarehe 20 Aprili 2025, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, baada ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kwa ukarabati. Maandalizi ya mchezo huu yamekamilika na timu ya Simba SC ipo tayari kupambana ili kufika fainali.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesisitiza kuwa Stellenbosch ni timu yenye nguvu na kufika kwake hatua hii ni ushahidi wa ubora wao. Kwa hivyo, Simba itahitajika kupigana kwa bidii ili kuhakikisha ushindi kwenye uwanja wa nyumbani. Kwa wale watakaotaka kushuhudia pambano hili la kihistoria, tiketi za kuingia uwanjani zimeanza kuuzwa rasmi na zinapatikana katika vituo mbalimbali Dar es Salaam na Zanzibar.
Vituo Rasmi vya Kununua Tiketi
Dar es Salaam
- Lampard Electronics – Simba HQ, Msimbazi
- Vunja Bei Shops – Maduka yote (Dar es Salaam)
- New Tech General Traders – Yeni Bar
- TTCL Shops – Dar es Salaam
- Juma Burrah – Msimbazi Center
- Halphani Hingaa – Oilcom Ubungo
- Mtemba Service Company – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo Rombo
- Mkaluka Traders Ltd – Machinga Complex
- Khalfani Mohammed – Ilala Bungoni
- Karoshy Pamba Collection – Dar Live
- Fusion Sports Wear – Posta DSM
- Gwambina Lounge – Temeke Opp Duce
- Antonio Service Co. – Sinza & Kivukoni
- Gisela Shirima – Dahomey Street
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sovereign Co. – Kinondoni Makaburini
- Gitano Samwel – Mbagala Zakhem
- Robert Nyabululu – Ferry Kigamboni
- Nicovic Enterprises Ltd – Segerea Oilcom
- Sabana Business Center – Mbagala Maji Matitu
- Tawi la Simba – Kariume Unstoppable
Zanzibar
- Amaan Stadium
- Mohamed Zahran Abdulla – Bandarini, Mkoani Pemba
- Shadrack Kimario – Kariakoo, Mchina Tambi
- Nuhu Jumanne Ally – Bububu Skuli
- Rashid Issa Juma – Fuoni (Mambo Sasa Nawasillisha)
- Lukuman Omar Khamis – Radio One, Daraja Bovu
- Harith – Amani
- Fahad – Kwerekwe
- Hamza – Melitano
- Suleiman – Kwerekwe Sokoni
- Hamid – Bububu
- Issa Yunus Issa – Fuoni Melinne
- Mwinyi Mwinyi Mwanakwerekwe – Car Wash
- TTCL Office – Kijangwani
