Michezo

Vita ya Aziz Ki na Fei Toto kwenye Tuzo za TFF leo Usiku

Vita ya Aziz Ki na Fei Toto kwenye Tuzo za TFF

Vita ya Aziz Ki na Fei Toto kwenye Tuzo za TFF

Aziz Ki na Feisal Salum, maarufu kama “Fei Toto,” wamekuwa wakichuana vikali katika msimu wa 2023/24, wakitafuta kutimiza malengo yao. Aziz Ki ameibuka kuwa mfungaji bora kwa mabao 21, akimzidi Fei Toto aliyefunga mabao 19.

Wachezaji hawa wawili, waliowahi kucheza pamoja Yanga, walionesha ustadi mkubwa ndani ya uwanja msimu uliopita. Aziz Ki aliongoza orodha ya wafungaji huku Fei Toto akifuatia kwa karibu. Mchuano wao uliendelea hadi mechi ya mwisho ya ligi, na wote walionyesha kiwango cha juu cha mchezo.

Katika tuzo za TFF za msimu wa 2023/24, Aziz Ki na Fei Toto wanachuana kwa nafasi ya Kiungo Bora na Mchezaji Bora wa Msimu. Usiku wa tuzo za TFF unafanyika leo katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar Es Salaam, ambapo mshindi ataamuliwa.

Nani ataibuka kidedea kati ya Aziz Ki na Fei Toto? Haya yatabainika usiku huu kwenye hafla ya kutangaza washindi wa tuzo za TFF.

Leave a Comment