Michezo

Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)

Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)

Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)

Wakati mashabiki wa vilabu vya soka barani Afrika wakisubiri kuanza kwa msimu mpya wa 2024/2025, klabu ya Al Ahly kutoka Misri imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya vilabu bora Afrika. Al Ahly, ambao wana historia ndefu ya mafanikio katika ulimwengu wa soka la Afrika, wameweza kushikiria nafasi yao kama klabu bora zaidi barani Afrika kutokana na mafanikio yao ya mara kwa mara katika michuano ya klaby bingwa ya CAF (CAF Champions league).

Klabu ya Esperance ya Tunisia imepanda hadi nafasi ya pili, ikipita Wydad Athletic Club ya Morocco baada ya kufanikiwa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2023/2024. Wydad, ambao walikuwa kwenye nafasi ya pili, wameporomoka hadi nafasi ya tatu baada ya kushindwa kufuzu kutoka kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa msimu huo.

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini imeendelea kushikilia nafasi ya nne, lakini inatarajiwa kushuka zaidi katika msimamo wa CAF kutokana na kushindwa kufuzu kwa michuano ya 2024/2025. Hii inaweza kuwa na matokeo kama yale yaliyoikumba klabu ya Raja Club Athletic ya Morocco, ambayo ilishuka kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya 12 baada ya kukosa kushiriki michuano ya CAF msimu uliopita.

Vilabu vingine vilivyo kwenye nafasi za juu katika msimamo wa Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking) ni pamoja na Zamalek ya Misri, RS Berkane ya Morocco, wekundu wa msimbazi Simba SC kutoka Tanzania, Petro de Luanda ya Angola, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), na CR Belouizdad ya Algeria.

Orodha ya Vilabu Bora Afrika kwa Msimu wa 2024/2025

  1. Al Ahly (Misri) – 87 alama
  2. Esperance (Tunisia) – 61 alama
  3. Wydad AC (Morocco) – 60 alama
  4. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) – 54 alama
  5. Zamalek (Misri) – 48 alama
  6. RS Berkane (Morocco) – 42 alama
  7. Simba SC (Tanzania) – 39 alama
  8. Petro de Luanda (Angola) – 39 alama
  9. TP Mazembe (DR Congo) – 38 alama
  10. CR Belouizdad (Algeria) – 36 alama

Hivyo ndio Vilabu Bora Afrika kwa msimu wa 2024/2025 (CAF Club Ranking)

Jinsi Ambavyo Viwango Hivi Vimepangwa

Kwa msimu wa 2024/2025 Vilabu Bora Afrika (CAF Club Ranking), alama zilizotumika kupangilia vilabu bora barani Afrika zimekusanywa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, yaani kuanzia 2019 hadi 2024. Alama zilizokusanywa kwa msimu wa 2023/2024 zimepewa uzito mkubwa zaidi, zikiwa zimezidishwa mara tano, wakati msimu wa 2022/2023 alama zake zimezidishwa mara nne, na msimu wa 2021/2022 mara tatu, msimu wa 2020/2021 mara mbili, na msimu wa 2019/2020 mara moja.

Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika hupata alama sita, ambapo Al Ahly wamepata alama 30 (6×5) kwa msimu wa 2023/2024. ES Tunis waliomaliza kama washindi wa pili walipata alama tano na hivyo kupata jumla ya alama 25 (5×5). Vile vile, vilabu vilivyofika hatua ya nusu fainali kama ASEC Mimosas na Mamelodi Sundowns vilipata alama nne, huku robo fainali zikipatiwa alama tatu, na timu zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi zikipewa alama mbili, na nafasi ya nne zikipata alama moja.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho la CAF, mshindi hupata alama tano, ambapo Zamalek walipata alama 25 (5×5). Washindi wa pili RS Berkane walipata alama nne na hivyo kufikisha alama 20 (4×5).

Leave a Comment