Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stellenbosch Aprili 20

0
Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stellenbosch Aprili 20

Simba SC Yatangaza Viingilio Mechi Dhidi ya Stellenbosch Aprili 20

Kuelekea pambano kali la Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kati ya Simba SC na Stellenbosch FC, klabu ya Simba imetangaza rasmi viingilio vya mchezo huo utakaochezwa Jumapili, Aprili 20, 2025 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Viingilio vya Mechi ya Simba vs Stellenbosch

Eneo la KukaaBei (Tsh)
VIP A40,000
VIP B20,000
Mzunguko10,000

NB: Tiketi zote zitauzwa kupitia mfumo wa N-Card pekee, na hakutakuwa na mauzo ya tiketi siku ya mechi nje ya uwanja.

Tangazo hilo limetolewa leo visiwani Zanzibar na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Ahmed alibainisha kuwa Uwanja wa Amaan una uwezo wa kuingiza watazamaji 15,885 pekee, hivyo ni muhimu kwa mashabiki kununua tiketi mapema.

Kwa mujibu wa Ahmed, tiketi kwa ajili ya VIP A zitauzwa kwa shilingi 40,000, VIP B kwa shilingi 20,000, huku mzunguko ukiuzwa kwa shilingi 10,000. Tiketi zote zitapatikana kwa njia ya kielektroniki kupitia mfumo wa N-Card, na hakuna tiketi zitakazouzwa kwa njia ya karatasi kama ilivyozoeleka huko nyuma.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam, vituo vyote vilivyozoeleka kuuza tiketi vitaendelea na huduma hiyo kama kawaida. Kwa upande wa Zanzibar, mashabiki wanashauriwa kujipatia N-Card mapema kwani mfumo huo ndio utakaotumika kikamilifu kwa mchezo huo.

Ahmed alisisitiza kuwa katika siku ya mechi hakutakuwa na mauzo ya tiketi nje ya uwanja au maeneo ya karibu, kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF). Mashabiki wote wanatakiwa kuhakikisha wanapata tiketi mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mchezo.

Mashabiki wa Simba na wapenda soka kwa ujumla wanahimizwa kufuata utaratibu huu mpya wa ununuzi wa tiketi kwa njia ya N-Card, ili kuhakikisha wanafurahia burudani ya soka bila kikwazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here