Ujio wa mchezaji mpya wa Yanga, Clatous Chota Chama, umewaletea shangwe mashabiki wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Chama amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba, ambapo alicheza kwa misimu sita tangu Julai Mosi, 2018, alipojiunga kutoka Klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia.
Usajili wa Chama ulileta gumzo kubwa nchini, kwani mashabiki wengi hawakuamini kuwa angehamia Yanga. Mwisho wa siku, Mwamba alihamia na kutambulishwa rasmi Jangwani.
Mbali na Chama, wachezaji wengine waliovutia hisia za mashabiki ni Prince Dube, aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kutoka Azam FC, pamoja na Pacome Zouzoua na Stephane Aziz KI.
Leave a Comment