HomeJamiiTuzo za TFF Zamchochea Tshabalala: Simba Kujipanga Upya kwa Mafanikio Msimu Ujao

Tuzo za TFF Zamchochea Tshabalala: Simba Kujipanga Upya kwa Mafanikio Msimu Ujao

Tuzo za TFF Zamchochea Tshabalala

Kitendo cha nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, kuwa mchezaji pekee aliyetwaa tuzo za TFF kutoka Msimbazi kwa timu ya wanaume, akiteuliwa kwenye Kikosi Bora cha Msimu cha Ligi Kuu Bara 2023-2024, kimemchochea beki huyo kuahidi maandalizi makali msimu ujao.

Tshabalala alishinda tuzo ya kuwemo kwenye kikosi bora cha msimu wa 2023/24, akisema kuwa tuzo hiyo inawapa nguvu kubwa wachezaji wa Simba kujitahidi zaidi, akiamini kuwa ligi ijayo itakuwa ya ushindi na mafanikio makubwa kwa timu yao.

“Katika maisha ya soka, ni kawaida kupokezana mafanikio. Simba tumekuwa tukinyakua tuzo hizi kwa miaka mingi, na hili linatupa nguvu mpya ya kupambana zaidi. Naamini msimu ujao utakuwa tofauti kabisa,” alisema Tshabalala, akirejea jinsi nyota wa Yanga walivyotawala tuzo hizo zilizofanyika juzi usiku jijini Dar es Salaam.

“Nafahamu mashabiki wetu wanapitia changamoto, lakini sasa ni wakati wa kusahau yaliyopita na kuungana kwa nguvu moja. Tuanzishe msimu mpya kwa ari ya kutafuta mafanikio ambayo tumeyakosa kwa miaka mitatu iliyopita,” aliongeza beki huyo wa kushoto wa Simba na Taifa Stars.

Mbali na Tshabalala, Kocha wa Simba Queens, Juma Mgunda, naye alipata tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL). Alisema, “Mafanikio haya yanatupa motisha ya kuandaa kikosi chetu kufanya vizuri katika michuano ya CAF. Shukrani kwa kila mmoja aliyeshiriki katika mafanikio haya.”

Simba Queens pia ilitoa Kipa Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Caroline Rufo, na Mfungaji Bora na Mchezaji Bora, Aisha Mnunka, pamoja na wachezaji walioteuliwa kwenye Kikosi Bora cha msimu wa ligi hiyo.

Kikosi Bora cha Msimu:

  • Ley Matampi
  • Yao Kouassi
  • Mohamed Hussein
  • Ibrahim Abdullah
  • Dickson Job
  • Mudathir Yahya
  • Maxi Nzengeli
  • Feisal Salum
  • Wazir Junior
  • Stephane Aziz Ki
  • Kipre Junior

Washindi wa Tuzo:

  • Mchezaji Bora Ligi Kuu Bara: Aziz Ki
  • Kiungo Bora Ligi Kuu Bara: Aziz Ki
  • Mfungaji Bora Ligi Kuu Bara: Aziz Ki
  • Beki Bora wa Ligi Kuu Bara: Ibrahim Bacca
  • Kipa Bora Ligi Kuu Bara: Ley Matampi
  • Mfungaji Bora Shirikisho: Clement Mzize
  • Mchezaji Bora Shirikisho: Feisal Salum
  • Kipa Bora Shirikisho: Diarra Djigui
  • Mchezaji Chipukizi Bara: Raheem Shomary
  • Mchezaji Chipukizi WPL: Ester Maseke
  • Kipa Bora WPL: Caroline Rufo
  • Mfungaji Bora WPL: Aisha Mnunka
  • Mchezaji Bora WPL: Aisha Mnunka
  • Kocha Bora Ligi Kuu: Miguel Gamondi
  • Kocha Bora WPL: Juma Mgunda
  • Mwamuzi Bora Bara: Ahmed Arajiga
  • Mwamuzi Bora WPL: Amina Kyando
  • Mwamuzi Msaidizi Bara: Mohammed Mkono
  • Mwamuzi Msaidizi WPL: Zawadi Yusuph
  • Tuzo za Rais TFF: Said El Maamry
  • Tuzo ya Heshima: Leodger Tenga
  • Tuzo ya Heshima WPL: Juma Bomba
  • Mchezaji Nje ya Nchi Wanaume: Mbwana Samatta
  • Mchezaji Nje ya Nchi Wanawake: Aisha Masaka
  • Mchezaji Bora Ufukweni: Jaruph Juma
  • Mchezaji Bora First League: Ayoub Masudi
  • Mchezaji Bora Championship: Edger William
  • Bao Bora la Msimu: Kipre Junior

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Posts