Michezo

Tiketi Za Simba Day 2024: Sold Out

Tiketi Za Simba Day 2024

Tiketi za Simba Day 2024 Zauzwa Kabla ya Wakati

Kwa mara nyingine, Klabu ya Simba imefanikiwa kuuza tiketi zote kwa ajili ya sherehe za Simba Day, zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya tukio ambalo litafanyika Jumamosi, tarehe 3 Agosti 2024, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mafanikio haya mapya yanaivunja rekodi iliyowekwa msimu uliopita ambapo tiketi zote ziliuzwa siku mbili kabla ya Simba Day, uwanja huo ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Imani Kajula, alieleza, “Simba tumeonyesha uwezo wetu mkubwa na kuvunja rekodi ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya Simba Day. Mwaka huu tumefanikisha kuuza tiketi zote siku tatu kabla – SOLD OUT.”

“Salamu zangu za pongezi kwa mashabiki wetu wote. Tukutane Uwanja wa Mkapa kwenye Simba Day ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya ‘Ubaya Ubwela’. Timu kubwa inapimwa kwa ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hili linaonyesha kwa nini mashabiki wa Simba walichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.”

Mashabiki wa Simba wanajulikana kwa kusema kazi yao ni kula, kulala na kuishabikia timu yao kwa moyo wote.

Leave a Comment