Tetesi za Usajili Ulaya Leo Jumatatu 19 Mei 2025
Manchester United Yawania Saini ya Mbeumo na Cunha
Klabu ya Manchester United ipo kwenye hatua za mwisho za kumalizana na mshambuliaji wa Wolverhampton, Matheus Cunha. Taarifa zinaeleza kuwa Cunha, raia wa Brazil, tayari ameridhia masharti binafsi na dili linaelekea kukamilika. Wakati huohuo, United imepeleka ofa ya euro milioni 65 kwa Brentford ili kumsajili Bryan Mbeumo, mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25 ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Liverpool Yaingia Sokoni kwa Milos Kerkez
Liverpool wameanza mazungumzo rasmi na klabu ya Bournemouth kwa ajili ya kumnasa beki wa kushoto Milos Kerkez. Mazungumzo ya awali yameonyesha mafanikio, huku pande zote mbili zikielekea kukubaliana kwenye ada ya uhamisho. Pia, Kerkez anaripotiwa kukubali kujiunga na klabu hiyo kwa masharti binafsi.

Kocha Francesco Farioli Aondoka Ajax
Katika hatua ya kushangaza, kocha mkuu wa Ajax, Francesco Farioli, ameamua kuachia ngazi mara moja. Uamuzi huo umetangazwa rasmi leo, huku Farioli akiwasilisha barua ya kujiondoa kwa uongozi wa klabu hiyo ya Uholanzi.
Cristiano Ronaldo Apokea Ofa Kutoka Brazil
Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Al-Nassr na nyota wa zamani wa Real Madrid, amepokea ofa ya kuvutia kutoka klabu moja ya Brazil. Ikiwa atakubali, Ronaldo mwenye umri wa miaka 40 atakuwa na nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia la Klabu litakalofanyika mwezi Juni.
Aston Villa Yamnyatia Ferran Torres wa Barcelona
Aston Villa inaripotiwa kuwa na nia ya kumsajili winga wa Barcelona, Ferran Torres. Klabu hiyo ya Ligi Kuu England ipo tayari kutoa takriban euro milioni 50 kwa nyota huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 25.
Juventus Kufungua Mlango kwa Dusan Vlahović
Mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahović, huenda akaondoka klabuni hapo msimu huu wa joto. Hakuna mazungumzo ya kuongeza mkataba wake ambao unakamilika mwaka 2026, hivyo uhamisho wake unaonekana kuwa uwezekano mkubwa zaidi.
Rayan Cherki Atangaza Kuondoka Lyon
Winga kinda wa Ufaransa, Rayan Cherki (21), ametangaza kuwa ataondoka Lyon msimu huu wa joto. Cherki amekuwa akiwaniwa na vilabu vya Premier League ikiwemo Manchester United na Liverpool.
United Yamfuatilia Pedro Goncalves wa Sporting
Mbali na Mbeumo na Cunha, Manchester United imeweka macho kwa kiungo wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Ureno, Pedro Goncalves, mwenye umri wa miaka 26. Kiungo huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri na anatajwa kuwa miongoni mwa vipaumbele vya United.
Leave a Comment