Man United Wamtamani Diogo Costa, Arsenal Wamnyatia Gyökeres – Tetesi za Usajili Ulaya Leo
Manchester United Wamtazama Diogo Costa Kuchukua Nafasi ya Onana
Manchester United wamewatuma wapelelezi kumfuatilia Diogo Costa, kipa wa FC Porto na timu ya taifa ya Ureno mwenye umri wa miaka 25, kama mbadala wa Andre Onana. Costa ana kipengele cha kutolewa cha pauni milioni 64.3, na pia anawindwa na Manchester City.
Arsenal Wamvizia Gyökeres na Nico Williams
Arsenal wameanza mazungumzo ya awali kwa nia ya kumsajili mshambuliaji wa Sporting CP na Uswidi, Viktor Gyökeres (26). Vilevile, winga wa Athletic Bilbao na timu ya taifa ya Hispania, Nico Williams (22), anachukuliwa kama kipaumbele ingawa bado hajakubali kuondoka.
Man City Wambakisha Kiungo Chipukizi O’Reilly
Nico O’Reilly (20), kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya vijana ya Uingereza, anatarajiwa kusaini kandarasi mpya licha ya Chelsea kuonyesha nia ya kumsajili.
United Wamrudia Benjamin Šeško
Manchester United wanaendeleza mawasiliano na wakala wa mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Šeško (21), ambaye alikataa kujiunga na klabu hiyo mwaka 2022. United wanataka kuhitimisha dili hilo dirisha lijalo la kiangazi.
Cunha Akaribia Kujiunga na Man Utd
United wapo hatua chache kufikia makubaliano ya kumsajili Matheus Cunha (25), mshambuliaji wa Wolves na Brazil. Hata hivyo, klabu hiyo inatakiwa kulipa kipengele cha pauni milioni 62.5 ili kukamilisha usajili huo.
Tottenham Wamnyatia Renato Veiga
Tottenham Hotspur wanapanga kutoa ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Chelsea na timu ya taifa ya Ureno, Renato Veiga (21), katika dirisha la kiangazi.
Harry Amass Kuvutwa kwa Mkopo
Manchester United wanatarajia ofa nyingi za mkopo kwa beki wa pembeni Harry Amass (18), anayekipiga katika kikosi cha England chini ya miaka 18.
Aston Villa Wataka Kumsajili Rashford
Aston Villa wanapanga kumuuza mshambuliaji wao Ollie Watkins (29) kwa kati ya pauni milioni 50-60 ili kufanikisha usajili wa Marcus Rashford (27) kwa mkataba wa kudumu kutoka Manchester United.
Xabi Alonso Karibu na Real Madrid
Bayer Leverkusen wako tayari kumuachia kocha wao Xabi Alonso endapo Real Madrid watamteua rasmi kuwa meneja wao mpya msimu wa joto.