Tanzania Yajibu Azimio la Bunge la Ulaya Mei 2025

0

Tanzania Yajibu Vikali Azimio la Bunge la Ulaya Mei 2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kauli rasmi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni majibu ya azimio la Bunge la Ulaya lililotolewa Mei 8, 2025, kuhusu masuala ya kisheria yanayoendelea nchini.

Katika taarifa hiyo, Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kulinda misingi ya katiba, kuheshimu uhuru wa mihimili ya dola, na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kujenga taifa jumuishi, lenye demokrasia na linalozingatia haki za binadamu.

Serikali pia imeeleza kuwa inatambua na kuthamini uhusiano wake wa muda mrefu na Umoja wa Ulaya, lakini imeonesha kutoridhishwa na namna baadhi ya wabunge wa Bunge hilo walivyotoa maamuzi bila kuzingatia usahihi wa taarifa au kutumia njia rasmi za kidiplomasia kujadili masuala hayo.

Serikali imetaja hatua hiyo kuwa ni ukiukwaji wa heshima kwa mamlaka ya kitaifa na ni kinyume na kanuni za kimataifa zinazotawala mahusiano kati ya nchi huru. Serikali imehimiza matumizi ya majadiliano ya moja kwa moja kama njia sahihi ya kutatua changamoto za kimataifa.

Tanzania Yajibu Vikali Azimio la Bunge la Ulaya Mei 2025
Tanzania Yajibu Vikali Azimio la Bunge la Ulaya Mei 2025
Tanzania Yajibu Vikali Azimio la Bunge la Ulaya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here