Tangazo La Nafasi Za Kazi – Sekretarieti Ya Ajira Katika Utumishi Wa Umma
Kumb. Na. JA.9/259/01/B/144
Tarehe: 27 Machi, 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 51 za kazi kwa niaba ya Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDA’s & LGA’s).
NAFASI ZA KAZI
1. MSAIDIZI WA AFYA (HEALTH ASSISTANT) – NAFASI 50
Majukumu ya Kazi:
- Kuchukua sampuli za maji na chakula kwa uchunguzi wa afya.
- Kutambua na kuhifadhi kumbukumbu za vyanzo vya maji.
- Kuandaa ramani za maeneo yaliyoathiriwa na uchafuzi wa maji.
- Kushirikiana na kamati za maji katika kulinda vyanzo vya maji.
- Kuhamasisha jamii kuhusu usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora.
- Kufanya ukaguzi wa nyumba za kuishi na biashara.
- Kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa kwa viongozi wa afya.
Sifa za Mwombaji:
- Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na ana cheti cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara:
- Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS – A.
2. MHANDISI MAZINGIRA DARAJA LA II (ENVIRONMENTAL ENGINEER II) – NAFASI 1
Majukumu ya Kazi:
- Kutoa ushauri kuhusu kulinda mazingira dhidi ya athari za shughuli za binadamu.
- Kufanya tathmini ya athari za mazingira (Environmental Impact Assessment).
- Kutoa ushauri juu ya udhibiti wa kemikali zinazotumika kwenye kilimo na viwanda.
- Kubuni vifaa na mbinu za kudhibiti uchafuzi wa mazingira.
- Kupendekeza mikakati ya kuhakikisha binadamu anaishi kwenye mazingira safi na salama.
Sifa za Mwombaji:
- Mwombaji awe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Uhandisi Mazingira kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Awe amesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).
Ngazi ya Mshahara:
- Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGS E.
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania na asiwe na umri zaidi ya miaka 45, isipokuwa walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na waeleze aina ya ulemavu wao katika mfumo wa maombi.
- Waombaji waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waambatishe CV yenye taarifa kamili pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Waombaji waambatishe nakala za vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ikiwa ni pamoja na:
- Vyeti vya kitaaluma (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates).
- Cheti cha mtihani wa kidato cha nne (Form IV) na sita (Form VI) kwa waliofikia kiwango hicho.
- Vyeti vya Kompyuta na vya kitaaluma kutoka bodi husika.
- Testmonials, Provisional Results, Statement of Results, na hati za matokeo za kidato cha nne na sita HAZITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTE).
- Waombaji waliostaafu katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba kazi hizi isipokuwa wawe na kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji walioajiriwa Serikalini kwenye nafasi za kuingilia hawapaswi kuomba kazi hizi.
- Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utasababisha hatua za kisheria.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
- Mwisho wa kutuma maombi ni 07 Aprili, 2025.
- Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani:
👉 http://portal.ajira.go.tz/ - Maombi yaliyo nje ya utaratibu huu hayatafanyiwa kazi.
Anwani ya kutuma maombi:
KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S. L. P. 2320, DODOMA
Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira na ingia kwenye sehemu ya Recruitment Portal.
Imetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Leave a Comment