Michezo

Skudu Ana Njia Mpya ya Kumvutia Gamondi

Skudu Ana Njia Mpya ya Kumvutia Gamondi

Mchezaji wa Yanga kutoka Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela, maarufu kama ‘Skudu’, amesema amegundua mbinu mpya ya kuhakikisha anapata muda zaidi wa kucheza kwenye timu hiyo.

Skudu Ajipata Yanga Ya Gamondi

“Kutokana na ushindani uliopo, nimebaini kuwa ili niwe na nafasi zaidi ya kucheza lazima niwe na kitu cha kipekee kila ninapopata fursa. Kila kocha anaponipa nafasi, ninalenga kuonyesha kuwa nilistahili kwa kufanya vizuri ili kupata nafasi zaidi,” alisema Skudu.

Msimu uliopita akiwa Yanga, Skudu hakuwa na nafasi nyingi za kucheza kutokana na ushindani mkali, na sasa kwa sababu Yanga imesajili wachezaji wapya, ushindani umeongezeka zaidi.

Kwa hiyo, msimu wa 2024/25 unaweza kuwa mgumu zaidi kwa Skudu kama hatabadilisha aina yake ya uchezaji. Timu ya Yanga chini ya kocha Gamondi inataka wachezaji wake wasikae sana na mpira au kufanya michezo isiyo na manufaa kwa timu. Skudu, ambaye mara nyingi anajulikana kwa uchezaji wake wa kufurahisha mashabiki, lazima abadili mbinu zake ili kufanikiwa zaidi.

Leave a Comment