Michezo

Simba Yaweka Juhudi kwa Mpanzu kwa Mara Nyingine

Simba Yaweka Juhudi kwa Mpanzu kwa Mara Nyingine

Wakati Simba ikiendelea na maandalizi yake ya kurejea nchini kutoka kambi yao ya Ismailia, Misri, mabosi wa klabu hiyo wamerejea tena kumjadili winga Ellie Mpanzu kutoka AS Vita. Mpanzu anatarajiwa kuziba nafasi ya Kibu Denis ambaye yuko kwenye mazungumzo ya kuhamia Norway.

Simba awali iliamua kuachana na Mpanzu na kumleta Willy Onana, ambaye alitarajiwa kujiunga na timu nchini Qatar ili kutimiza idadi ya wachezaji wa kigeni wasiozidi 12 kwa timu moja.

Hata hivyo, Mwanaspoti imepata habari kutoka ndani ya klabu hiyo kwamba endapo Simba itakamilisha mchakato wa kumsajili Mpanzu, Onana anaweza kumpisha. Iwapo Onana hatakwenda Qatar, basi Freddy Michael atakuwa mchezaji anayetarajiwa kuachia nafasi.

“Tumerejea tena kwa Mpanzu, ambaye tunaamini ana kasi na uwezo wa juu kama Kibu. Ingawa suala la Kibu bado halijakamilika, kwani timu anayotarajiwa kujiunga nayo inahitaji kumnunua moja kwa moja badala ya kumchukua kwa mkopo au majaribio ya mwezi mmoja,” chanzo hicho kilisema Mwanaspoti na kuongeza:

“Ni kweli dau la Mpanzu ni kubwa na ndilo lililoturudisha nyuma, lakini tunaendelea kupambana kukamilisha usajili wake kwa sababu tunaweza tusimwone Kibu kikosini msimu ujao, na tunaamini Mpanzu ataweza kuisaidia timu kwa kiasi kikubwa.”

Chanzo hicho kiliendelea kusema kwamba kocha mkuu Fadlu Davis anajua kinachoendelea na anafuatilia kila hatua, akiamini kuwa Mpanzu ni mchezaji mzuri.

“Kocha anafahamu kila kinachoendelea na amemwona Mpanzu kama mchezaji mzuri, ndio maana tumeongeza juhudi kuhakikisha tunampata na awe sehemu ya kikosi chake,” kilisema chanzo hicho.

Leave a Comment