Klabu ya Simba ilijitahidi sana kuipata saini ya winga machachari wa AS Vita, Elie Mpanzu. Ingawa walimshawishi mchezaji kwa ahadi za masilahi mazuri, AS Vita ilionekana kubadilika mara kwa mara katika kuamua hatima yake, ikionyesha kuwa hawakuwa na mpango wa kumuuza.
Simba Isilaumiwe Kumkosa Elie Mpanzu
Awali, AS Vita walidai dau ambalo Simba ilikuwa tayari kulipa, lakini baadaye walidai changamoto ya umiliki wa mchezaji, hivyo wakataka fedha zaidi. Simba ilikubali kulipa hata dau la pili, lakini AS Vita iliendelea kuwazungusha kwa sababu zisizoeleweka.
Mwishowe, Simba iliamua kuacha kumsajili Mpanzu kwani AS Vita haikuwa na utayari wa kumwachia. Ghafla, tumesikia Mpanzu amehamia Ubelgiji na yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na KRC Genk.
Inaonekana AS Vita ilikuwa inajua kuhusu mpango wa Mpanzu kuhamia Genk, ndiyo maana walikuwa wanawazungusha Simba. Kiungwana ingekuwa bora wawaachie Simba mapema ili watafute mchezaji mwingine kabla ya muda wa usajili kumalizika.
Leave a Comment