Michezo

Simba Wakwama Na Usajili Wa Awesu, Kagoma: Kivumbi TFF

Simba Wakwama Na Usajili Wa Awesu, Kagoma

Sakata la usajili wa Awesu na Kagoma latikisa Simba SC, TFF wakutana kujadili malalamiko kutoka Yanga na KMC, huku Simba wakipigwa stop.

Simba Wakwama Na Usajili Wa Awesu, Kagoma

Sakata la usajili limekuwa gumu kwa Simba SC, ambapo nyota wapya Awesu Awesu, Yusuf Kagoma, na Valentino Mashaka wameingiza klabu hiyo kwenye mgogoro na TFF. Wachezaji hao waliosajiliwa kutoka KMC, Singida Fountain Gate, na Geita Gold, wamewekewa pingamizi na klabu zao za zamani, jambo lililopelekea Simba kushindwa kuwatumia kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, ambapo walipoteza kwa bao 1-0 lililofungwa na Maxi Nzengeli.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilikutana jana kujadili mashauri yaliyowasilishwa, likiwemo sakata la Kagoma na Awesu. Kagoma anatuhumiwa kusajiliwa na Simba wakati Yanga ikidai kuwa walishalipa pesa kwa Singida Fountain Gate ili kumsajili kiungo huyo, lakini Simba ikaingia naye mkataba wa miaka miwili. Chanzo cha karibu kimethibitisha kuwa Yanga walitoa fedha kwa klabu ya Kagoma, lakini baada ya mchezaji huyo kujiunga na Simba, fedha hizo hazijarejeshwa.

Kwa upande wa Awesu, kocha Fadlu Davids alikuwa amempanga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, lakini Simba ilipata taarifa kutoka Bodi ya Ligi kuwa mchezaji huyo haruhusiwi kucheza kutokana na malalamiko kutoka KMC, klabu yake ya zamani. Taarifa zinaeleza kuwa Awesu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na KMC, hivyo klabu hiyo ilifungua kesi TFF ikipinga usajili wake Simba.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungura, amethibitisha kuwa klabu yake imewashtaki Awesu na Simba kwa TFF kwa kukiuka taratibu za usajili, na kesi hiyo itasikilizwa leo.

Leave a Comment