Simba SC Yatinga Top 4 Afrika! Yawa Tishio CAF 2024/25

0
Simba SC Yatinga Top 4 Afrika! Yawa Tishio CAF 2024/25

Baada ya hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup kwa msimu wa 2024/2025, viwango vipya vya ubora wa vilabu Afrika vimetolewa, na kwa mara ya kwanza Simba SC kutoka Tanzania imeingia ndani ya klabu nne bora barani Afrika.

Simba SC Yatinga Top 4 Afrika

Simba SC imefanikiwa kukusanya jumla ya pointi 43, hatua iliyoiinua kutoka nafasi ya 6 hadi ya 4, baada ya kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu huu.

Kwa sasa, Simba SC inazidiwa tu na miamba watatu wa soka barani Afrika: Al Ahly ya Misri inayoongoza kwa alama 78, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance de Tunis ya Tunisia ambazo zote zina pointi 57.

Vilabu vingine vilivyopo kwenye nafasi ya juu ya msimamo huo ni kama ifuatavyo: RS Berkane (Morocco) na Zamalek (Misri) zote zikiwa na pointi 42 kila moja, zikifuatiwa na Wydad Athletic ya Morocco (39), Pyramids FC (37), USM Alger (37), na CR Belouizdad (36).

Yanga SC, bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inashikilia nafasi ya 11 barani Afrika kwa pointi 34, ikiwa ni hatua kubwa katika maendeleo ya klabu hiyo kwenye soka la kimataifa.

📊 Orodha Kamili ya Vilabu 30 Bora Afrika CAF 2024/2025:

  1. Al Ahly – Misri = 78
  2. Mamelodi Sundowns – Afrika Kusini = 57
  3. Esperance de Tunis – Tunisia = 57
  4. Simba SC – Tanzania = 43
  5. RS Berkane – Morocco = 42
  6. Zamalek – Misri = 42
  7. Wydad Athletic – Morocco = 39
  8. Pyramids FC – Misri = 37
  9. USM Alger – Algeria = 37
  10. CR Belouizdad – Algeria = 36
  11. Yanga SC – Tanzania = 34
  12. ASEC Mimosas – Ivory Coast = 33
  13. Al Hilal Omdurman – Sudan = 32
  14. TP Mazembe – DR Congo = 30.5
  15. Orlando Pirates – Afrika Kusini = 30
  16. Raja Casablanca – Morocco = 30
  17. Petro de Luanda – Angola = 27
  18. AS FAR Rabat – Morocco = 21
  19. MC Alger – Algeria = 18
  20. Sagrada Esperanca – Angola = 16
  21. CS Constantine – Algeria = 15
  22. Stellenbosch FC – Afrika Kusini = 15
  23. Al Masry – Misri = 14
  24. Rivers United – Nigeria = 14
  25. JS Kabylie – Algeria = 13
  26. Dreams FC – Ghana = 12
  27. Stade Malien – Mali = 10.5
  28. Horoya Athletic – Guinea = 10
  29. Future FC – Misri = 9.5
  30. Etoile du Sahel – Tunisia = 9

Kupanda kwa Simba na Yanga kwenye viwango hivi ni ishara kuwa soka la Tanzania linazidi kusimama imara kwenye ramani ya soka Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here