Michezo

Simba SC inataka Bilioni 2 Kumuachia Kibu Denis… Akana Mwanasheria Wake

Simba SC inataka Bilioni 2 Kumuachia Kibu Denis… Akana Mwanasheria Wake

Baada ya Kibu Denis, winga aliyekimbilia Ulaya, kumkana mwanasheria wake Rashid Yazid na kudai kumtambua meneja wake Carlos MasterMind pekee, habari mpya zimeibuka kuhusu mchezaji huyo anayefanya majaribio nchini Norway.

Klabu ya Kristiansund BK ya Norway imeandika barua kwa Simba SC ikimwomba Kibu Denis kwa ajili ya majaribio, huku ikikiri kuwa haikujulishwa ukweli kuhusu mchezaji huyo. Hali hii ilisababisha wao kufanya makosa ya kuwasiliana na kumtumia mwaliko mchezaji ambaye bado ana mkataba unaozidi miezi sita bila kwanza kuwasiliana na klabu na kupata ruhusa ya kuwasiliana na mchezaji huyo.

Klabu hiyo ya Norway pia imethibitisha kuwa imekiuka taratibu na kanuni za FIFA na kuona hatari iliyopo mbele yao. Simba SC wako tayari kumuachia Kibu Denis aondoke lakini wanataka kipengele cha kuuzwa mchezaji kifikiwe, ambacho ni dola za Kimarekani milioni 1 ($1M) sawa na bilioni 2.7 za Kitanzania (Tshs 2.7B).

Simba SC hawataki kusikia kuhusu majaribio kwa sababu kuna uwezekano wa kupata au kukosa, na iwapo akakosa na kurudi, watakuwa wamewapa mwanya wachezaji wao kuondoka kihuni. Kristiansund BK wanaona bilioni 2.7 ni nyingi sana na wanataka suluhu, lakini Simba wanataka heshima yao iliyopotezwa irudishwe.

Ingawa uzoefu unaonyesha kuwa Simba ni klabu inayowaachia wachezaji kwenda nje kucheza wanapopata nafasi, katika hili, pia watafikia mwisho na Kibu Denis atapata nafasi kucheza Ulaya na kutimiza ndoto zake.

Leave a Comment