Michezo

Simba na Yanga Kukutana Okt 19! Bodi ya Ligi Yatangaza Ratiba Mpya

Simba na Yanga Kukutana Okt 19! Bodi ya Ligi Yatangaza Ratiba Mpya

Ratiba ya Msimu Mpya wa Ligi Kuu 2024/25

Bodi ya Ligi hatimaye imetangaza ratiba ya Msimu wa Ligi Kuu 2024/25, ambapo msimu utaanza rasmi Agosti 16 kwa mchezo mmoja tu. Simba SC wataanza kampeni zao za ligi tarehe 18 Agosti dhidi ya Tabora Utd, mechi ambayo itafanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, ambao Simba wameuchagua kama uwanja wao wa nyumbani kwa michezo kadhaa msimu huu. Hata hivyo, mechi kubwa zitaendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga SC, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, wataanza safari yao ya kutetea ubingwa kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba. Yanga pia wameamua kutumia Uwanja wa Azam Complex kwa sehemu kubwa ya mechi zao za nyumbani msimu huu.

Azam FC watacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Mej. Jen. Isamuhyo.

Mechi 10 za Awali za Simba SC 2024/25:

  1. Simba vs Tabora Utd
  2. Simba vs Fountain Gate
  3. Tz Prisons vs Simba
  4. Azam FC vs Simba
  5. Simba vs Namungo
  6. Dodoma Jiji vs Simba
  7. Simba vs Coastal Union
  8. Simba vs Yanga – Oktoba 19
  9. Mashujaa FC vs Simba
  10. Simba vs JKT Tanzania

Mechi 10 za Awali za Yanga SC 2024/25:

  1. Kagera Sugar vs Yanga
  2. KenGold FC vs Yanga
  3. Yanga vs JKT Tanzania
  4. Yanga vs Mashujaa FC
  5. Singida BS vs Yanga
  6. Yanga vs KMC FC
  7. Yanga vs Pamba Jiji
  8. Simba vs Yanga – Oktoba 19
  9. Yanga vs Tabora Utd
  10. Coastal Union vs Yanga

Simba na Yanga Kukutana Okt 19!

Macho yote yanatarajiwa kuelekezwa kwenye pambano kati ya Simba na Yanga litakalopigwa Oktoba 19, ikiwa ni mechi ya nane kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC. Mechi hii itakuwa kipimo kikubwa cha nguvu kati ya wapinzani hawa wakubwa.

Leave a Comment