Mwandishi maarufu wa habari nchini Tanzania, Saleh Jembe, ametoa maoni yake kuhusu Kibu Denis, kiungo mshambuliaji wa Simba, akisema hakupaswa kucheza katika mchezo wa Simba Day. Tarehe 3 Agosti 2024, Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda 2-0 dhidi ya APR, na miongoni mwa wachezaji waliocheza ni Kibu, Mohamed Hussen, Ally Salim, na Edwin Balua.
Jembe amesema: “Kibu hakustahili kucheza ile mechi kwa kuwa amewakosea sana Simba na kuzomewa na mashabiki alistahili kwani kitendo alichofanya ilikuwa ni cha hovyo. Alijua kuwa ana mkataba na fedha za Simba lakini hakujiunga na timu kambini.”
“Inasemekana kuwa kocha alitaka kumuona Kibu akicheza, lakini tumeona jinsi alivyokuwa hafiti kabisa na alicheza vibaya hivyo hakupaswa kabisa kucheza mchezo ule.”
Kibu hakuwa na Simba kambini nchini Misri na alirejea timu ikiwa Bongo. Alifanya mazoezi na timu siku moja kabla ya mchezo wa Simba Day uliochezwa Agosti 3, 2024, ambapo Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR, mabao yaliyofungwa na Deborah Fernandes na Edwin Balua.
Leave a Comment