RATIBA ya Mechi za Simba Zilizobaki 2025
Ushiriki wa Simba SC Katika Mashindano Mei 2025
Klabu ya Simba itacheza mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ya NBC pamoja na Kombe la Shirikisho mwezi Mei 2025. Hatua hii inatokana na ushiriki wao katika Kombe la Shirikisho la CAF ambapo mchezo wa Nusu Fainali Mkondo wa Pili dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini utafanyika April 27, 2025.
Ratiba Kamili ya Mechi za Simba Mei 2025
Hii hapa ratiba kamili ya mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu ya NBC na CRDB Bank Federation Cup:
- May 02, 2025 – NBC Premier League
16:00 Simba SC vs Mashujaa FC - May 05, 2025 – NBC Premier League
16:00 JKT Tanzania vs Simba SC - May 08, 2025 – NBC Premier League
16:00 Simba SC vs Pamba Jiji FC - May 11, 2025 – NBC Premier League
16:00 KMC FC vs Simba SC (Tabora) - May 14, 2025 – NBC Premier League
16:00 Simba SC vs Singida Black Stars - May 21, 2025 – NBC Premier League
16:00 KenGold FC vs Simba SC - May 25, 2025 – NBC Premier League
16:00 Simba SC vs Kagera Sugar FC - TBD 2025 – NBC Premier League
TBA Yanga SC vs Simba SC
Aidha, mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars pia unatarajiwa kuchezwa kati ya May 16-18, 2025.
Maendeleo ya Simba SC Kimataifa
Iwapo Simba SC itafuzu Fainali ya CAF Confederation Cup 2024/2025, mchezo wa Fainali utaongezeka kwenye ratiba kulingana na tarehe zitakazopangwa na CAF.
Mechi za Simba SC Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 2025
Katika mwezi wa Mei 2025, Simba SC inatarajiwa kucheza michezo muhimu ya ligi kuu ambayo itakuwa na mchango mkubwa katika kuamua hatima yao ya ubingwa wa msimu huu. Ratiba hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia tarehe rasmi zilizotangazwa na Bodi ya Ligi.