Elimu

Plate Namba za Magari ya Serikali Tanzania

Plate Namba za Magari ya Serikali Tanzania

Plate Namba za Magari ya Serikali Tanzania na Maana Yake

Katika Tanzania, magari yana namba za kipekee za usajili zinazosaidia katika utambulisho na ufuatiliaji barabarani. Magari ya serikali yana namba maalum zinazojulikana kama “Plate Number za Magari ya Serikali”.

Aina za Plate Namba za Serikali

Viongozi Wakuu wa Serikali na Mihimili Mikuu Mitatu:

  • Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu: Magari yao hutambulika kwa nembo ya Taifa ya Bwana na Bibi badala ya namba.
  • Spika wa Bunge na Naibu Spika: Magari haya hutumia herufi “S” kwa Spika na “NS” kwa Naibu Spika.
  • Katibu Mkuu Kiongozi: Gari lake hutumia herufi “CS”.
  • Jaji Mkuu: Hutumia herufi “JM”.
  • Mkuu wa Majeshi: Magari haya yana nyota nne badala ya namba.

Mawaziri na Maafisa Wengine:

  • Mawaziri na Manaibu Waziri: Hutumia herufi “W” kwa Waziri na “NW” kwa Naibu Waziri.
  • Wakuu wa Mikoa: Hutumia herufi “RC” ikifuatiwa na kifupisho cha mkoa, kama “RC-DSM” kwa Dar es Salaam.

Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma, na Vyombo vya Ulinzi:

  • Serikali za Mitaa: Hutumia herufi “SM” ikifuatiwa na namba.
  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar: Hutumia herufi “SMZ”.
  • Mashirika ya Umma: Kama TANESCO na DAWASA, hutumia herufi “SU”.
  • Polisi, Jeshi, na Magereza: Hutumia herufi “PT” kwa polisi, “JW” kwa jeshi, na “MT” kwa magereza.

Plate Namba za Kipekee:

  • Miradi ya Wahisani: Hutumia herufi “DFP” au “DFPA”.
  • Ubalozi na Mashirika ya Kimataifa: Hutumia herufi “T” ikifuatiwa na “CD”.

Leave a Comment