HomeMichezoPesa za Zawadi za CAF Confederation Cup 2024/2025

Pesa za Zawadi za CAF Confederation Cup 2024/2025

Thamani ya Kombe La Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup)

Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) linachukua nafasi ya pili kwa ukubwa baada ya CAF Champions League barani Afrika. Mashindano haya yanapitia mabadiliko makubwa yatakayoimarisha thamani na mvuto wake. Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, ametangaza ongezeko kubwa la zawadi za fedha kwa washindi na washiriki, likiwa lengo la kuboresha mashindano na kusaidia vilabu vinavyoshiriki.

Pesa za Zawadi za CAF Confederation Cup

Kwa mara ya kwanza, zawadi kwa mshindi wa Kombe la Shirikisho Afrika imeongezeka kutoka dola milioni 1.2 hadi dola milioni 2. Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha thamani ya mashindano na kuvutia vilabu zaidi kujiunga. Hapa kuna muhtasari wa zawadi za fedha kwa hatua mbalimbali za mashindano:

  • Mshindi: Dola milioni 2
  • Mshindi wa Pili: Dola milioni 1
  • Nusu Fainali: Dola 750,000
  • Robo Fainali: Dola 550,000
  • Nafasi ya 3 Katika Kundi: Dola 400,000
  • Nafasi ya 4 Katika Kundi: Dola 400,000

Kwa mara ya kwanza katika historia, CAF itatoa msaada wa kifedha kwa vilabu vinavyoshiriki katika hatua za awali. Kila klabu itakayoingia raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho itapokea dola 50,000. Hii itasaidia kupunguza gharama za usafiri na vifaa, na kuwezesha vilabu vya rasilimali chache kushiriki katika mashindano haya ya kimataifa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Posts