Katika maandalizi ya mechi ya dabi itakayofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua, amezungumzia kwa kina kuhusu mwanzo wake mpya na matarajio yake.
Pacome Zouzoua, ambaye ni nyota wa kimataifa kutoka Ivory Coast, amesisitiza kuwa anatarajia mashabiki wa Yanga kufurahia kiwango chake katika mchezo wa Agosti 8 dhidi ya Simba SC. Ameongeza kuwa kocha Miguel Gamondi amewaeleza wachezaji kuwa hatangalia majina maarufu bali ubora wao uwanjani.
Zouzoua amesema, licha ya ushindani mkali wa nafasi ndani ya timu, anataka kuleta tofauti na kuhakikisha anapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake. “Mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wetu kuwa na wachezaji bora na wenye rekodi nzuri,” amesema Zouzoua.
Anakumbuka kuwa msimu uliopita alishiriki kwenye mechi za Derby ambapo Yanga iliwafunga Simba kwa jumla ya mabao 7-2 katika mechi mbili. Hata hivyo, msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kwa sababu ya majeraha yaliyopelekea kushindwa kucheza mechi mbili muhimu za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Kwa mujibu wa Zouzoua, Yanga inajua umuhimu wa kupata matokeo mazuri katika mechi kubwa kama hii, na ana matumaini kwamba timu itafanya vizuri na kuwa na mwanzo mzuri wa msimu mpya.
Leave a Comment