Ajira Tanzania

Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo TRA, 23 March 2025

Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo TRA, 23 March 2025

Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo pdf, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo TRA 2025, Call For interview TRA 2025. TRA SELECTED NAMES FOR WRITTEN INTERVIEW. 

Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995, na ilianza
kufanya kazi tarehe 1 Julai 1996 na kukasimiwa Mamlaka ya Kutathimini, Kukusanya na kuhasibu
mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria. Katika kuhakikisha kuwa Mamlaka inatimiza kusudi la
kuanzishwa kwake imekuwa ikiandaa na kutekeleza mipango kazi wa miaka mitano mitano, aidha
kwasasa TRA inatekeleza mpango kazi wa sita (CP6:2022/23 – 2026/27) wenye Dira ya kuwa ‘‘Taasisi
ya Mapato Inayoaminika kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi’’ na Dhamira ya ‘‘Kurahisisha na
Kuimarisha Ulipaji Kodi wa Hiari kwa Maendeleo Endelevu’’.
TRA inapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuanzia tarehe 06 Februari, 2025
mpaka 19 Februari, 2025 kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kwa hatua mbalimbali kuanzia tarehe

29 Machi, 2025. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

  1. Usaili utafanyika kwa tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili ikiainisha siku, muda na
    sehemu ambapo usaili utafanyika kwa kila Kada.
  2. Kila Msailiwa anapaswa kufika na barua ya kuitwa kwenye usaili yenye namba ya mtahiniwa
    iliyotumwa kwenye anuani yake ya barua pepe. Namba hiyo itatumika wakati wa usaili.
  3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho
    vinavyokubalika ni pamoja na: – Kitambulisho cha Uraia, Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho
    cha Mpiga Kura, Leseni ya Udereva, Hati ya kusafiria au Barua ya Utambulisho kutoka Serikali
    ya Mtaa/Kijiji unachotoka. Vitambulisho Tofauti na Vilivyoainishwa Havitatambuliwa.
  4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (Original certificates) kuanzia Cheti
    cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada
    na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji. Pia Wasailiwa wote wanatakiwa kufika na
    nakala (Photocopy) za vyeti vya kitaaluma pamoja na hati za matokeo za vyuo
    (Transcript).
  5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, Transcript,
    hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) bila kuwa na vyeti halisi
    HAWATAKUBALIWA KUENDELEA NA USAILI.
  6. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na
    kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
  7. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao
    Halisi vya Usajili na Leseni za kufanyia kazi (kwa wanaohusika).
  8. Msailiwa ataruhusiwa kufanya usaili baada ya kukamilisha uhakiki wa vyeti na kukidhi sifa za
    kazi aliyoomba.
  9. Uhakiki wa vyeti utaanza Saa 12.00 Asubuhi kwa ratiba ya asubuhi na Saa 6.00 Mchana kwa
    ratiba ya mchana.
  10. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  11. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na kituo alichopangiwa kufanyia usaili.
  12. Msailiwa haruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la usaili.
  13. Wasailiwa wenye mahitaji maalum wanashauriwa kufika mapema na kuripoti kwa Msimamizi wa
    Kituo ili kupatiwa msaada utakaohitajika.
  14. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
    hawakukidhi vigezo vya awali. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
    zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
    Kwa taarifa zaidi tumia mawasiliano yafuatayo:
    Tovuti : www.tra.go.tz
    Namba za simu bila malipo : 0800 780078 au 0800750075
    WhatsApp : 0744 23 33 33
    Barua pepe : [email protected] au [email protected]
    ‘‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’’
    Imetolewa na;
    Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA

Leave a Comment