HomeMichezoOnana Abaki Simba SC Baada ya Dili la Qatar Limekufa

Onana Abaki Simba SC Baada ya Dili la Qatar Limekufa

Dili la Onana Kwenye Klabu ya Qatar Lafeli Rasmi

Uhamisho wa mchezaji wa Simba SC, Willy Esomba Onana kwenda Qatar umeshindwa kufanikiwa baada ya uongozi na kamati ya usajili kumjadili kwa kina mchezaji huyo.

Katika klabu za Qatar, mchezaji anayependekezwa husajiliwa baada ya kamati maalum kukaa na kumjadili mchezaji huyo kwa undani na kuchukua uamuzi wa mwisho. Hii kamati huchambua mambo kadhaa kama vile fomu ya wachezaji, malengo na usaidizi, na rekodi za matibabu au majeraha.

Inaonekana kamati hiyo haikuridhishwa na kiwango cha Onana na hawana uhakika kama anaweza kufanikiwa kwenye ligi ya Qatar. Kwa hiyo, wamependekeza kutokuendelea na mpango wa kumsajili.

Kutokana na uhamisho huo kushindikana, Onana atalazimika kurejea Simba SC, klabu yake ya awali ambayo ana mkataba nayo. Simba SC itabidi imtafutie klabu nyingine kama Onana hatohitajika tena kwenye kikosi chao.

Onana aliondoka Simba na nafasi yake ilichukuliwa na kipa mpya, Musa Camara. Hata hivyo, inaonekana Simba SC inaweza kumtoa Ayoub Lakred ili Onana abakie, maana bado anatakiwa kubaki Simba SC Tanzania.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Posts