Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 29, 2024.
Matokeo hayo yametolewa rasmi leo, Alhamisi, Januari 23, 2025, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohammed.
Wanafunzi pamoja na wazazi sasa wanaweza kuyaona matokeo hayo kupitia tovuti rasmi ya NECTA.
Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024/2025
NECTA: Matokeo Kidato Cha Nne 2024/2025 Form Four Results
Hongera kwa waliofanikiwa, na kwa wale ambao hawakufikia malengo, bado kuna nafasi ya kujifunza na kufanikiwa zaidi!
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.
Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.
Aidha, Baraza la Mitihani limetangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi kwenye mitihani.
Dk Said Mohammed amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili.
“Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,”
Leave a Comment