Namna Rahisi ya Kupata Namba ya NIDA (NIN) Bila Usumbufu
Namba ya NIDA ni nyaraka muhimu kwa kila Mtanzania kwani hutumika kuthibitisha utambulisho katika shughuli nyingi rasmi. Namba hii hutolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia na wakazi wa kigeni walioko Tanzania.
Katika miaka ya hivi karibuni, namba hii imekuwa ya lazima katika kufungua akaunti ya benki, kusajili laini za simu, kupata huduma za kijamii, na shughuli nyingine za serikali au binafsi.
Umuhimu wa Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka
Kwa kuwa huduma nyingi sasa zinategemea uwe na Namba ya NIDA, ni muhimu kuhakikisha unaipata mapema iwezekanavyo. Hata kama bado hujapokea kadi ya NIDA, namba yako inaweza kutumika kuthibitisha utambulisho wako katika taasisi mbalimbali. Kupata namba hii mapema kunakupa fursa ya kupata huduma kwa urahisi na haraka.
Namna ya Kupata Namba ya NIDA Kupitia Simu ya Mkononi
NIDA imerahisisha mchakato wa kupata namba kwa kutumia simu. Hii inamaanisha kuwa huhitaji kwenda ofisini, unaweza kupata huduma ukiwa nyumbani. Fuata hatua hizi:
- Piga 15200# kwenye simu yako.
- Chagua namba 3: Ajira na Utambuzi.
- Kisha chagua namba 2: Huduma za NIDA.
- Ingiza majina yako matatu kama yalivyo kwenye fomu ya usajili. Mfano: Dan John Sele.
- Weka namba ya simu uliyotumia kusajili NIDA.
- Hakiki taarifa zako kisha thibitisha kwa kubofya βKubali.β
Huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa mitandao ya Vodacom na Airtel.
Namna ya Kupata Namba ya NIDA Mtandaoni (Online)
Kupitia intaneti, unaweza kujua Namba yako ya NIDA bila kusafiri kwenda ofisini. Unahitaji:
- Majina Kamili (Kama yalivyo kwenye usajili)
- Tarehe ya Kuzaliwa (Mfano: 01-01-1990)
- Majina ya Mama (Jina la kwanza na la mwisho)
- Muunganisho wa intaneti
Hatua za Kufuatilia:
- Tembelea tovuti rasmi ya NIDA:
π https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin.aspx - Tafuta sehemu iliyoandikwa “Know Your Number (NIN)” upande wa kushoto wa tovuti.
- Jaza fomu kwa taarifa zako sahihi:
- Jina la Kwanza
- Jina la Mwisho
- Tarehe ya Kuzaliwa
- Jina la Kwanza la Mama
- Jina la Mwisho la Mama
- Hakiki usalama: Weka namba au maandishi yanayoonekana ili kuthibitisha kuwa wewe si roboti.
- Bonyeza βTUMAβ ili kuwasilisha taarifa zako.
- Ukijaza taarifa zote kwa usahihi, namba yako ya NIDA itaonekana kwenye skrini. Iandike au ihifadhi mahali salama.
Njia Mbadala za Kupata Namba ya NIDA kwa Haraka
Iwapo unapata changamoto kutumia simu au intaneti, kuna njia nyingine unazoweza kutumia:
1. Piga Simu Kituo cha Huduma kwa Wateja
Unaweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa NIDA kupitia namba zifuatazo:
- 0752 000 058
- 0687 088 888
- 0777 740 006
- 0677 146 666
2. Tembelea Ofisi za NIDA
Kama unapendelea kufuatilia taarifa zako moja kwa moja, unaweza kwenda kwenye ofisi ya NIDA iliyo karibu nawe kwa msaada zaidi.
Mawasiliano Zaidi ya NIDA
- Simu: 0759 102010 / 0765 201020 / 0673 333444 / 0800758888
- Barua Pepe: [email protected]
- Tovuti: nida.go.tz
Kupata Namba ya NIDA kwa haraka sasa ni rahisi zaidi kuliko hapo awali, na unaweza kufanya hivyo bila kulazimika kusubiri kwa muda mrefu.