Aziz Ki ameacha mashabiki wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na mshangao mkubwa kutokana na namba zake za kutisha. Tangu mwaka 2004, wachezaji mbalimbali wamekuwa wakishindania kiatu cha dhahabu, lakini hakuna aliyeweza kufikia rekodi aliyoweka Aziz Ki.
Wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara tangu mwaka 2004 hadi sasa (miaka 20) ni:
- 2005 – Abu Mkangwa (Mtibwa) – 16
- 2006 – Isse Abshir (Simba) – 19
- 2007 – Abdallah Juma (Mtibwa) – 20
- 2008 – M. Katende (Kagera) – 11
- 2009 – Boni Ambani (Yanga) – 18
- 2010 – Mussa Mgosi (Simba) – 18
- 2011 – Mrisho Ngassa (Azam) – 18
- 2012 – John Bocco (Azam) – 19
- 2013 – Kipre Tchetche (Azam) – 17
- 2014 – Amiss Tambwe (Simba) – 19
- 2015 – Simon Msuva (Yanga) – 17
- 2016 – Amiss Tambwe (Yanga) – 21
- 2017 – Simon Msuva & Abdulrahman – 14
- 2018 – Emmanuel Okwi (Simba) – 20
- 2019 – Meddie Kagere (Simba) – 23
- 2020 – Meddie Kagere (Simba) – 22
- 2021 – John Bocco (Simba) – 16
- 2022 – George Mpole (Geita) – 17
- 2023 – Fiston Mayele & Saidi Ntibazonkiza – 17
- 2024 – Stephane Aziz Ki (Yanga) – 21
Katika miaka ya hivi karibuni, mfumo wa timu 16 ulirejea msimu wa mwaka 2021/22, na hakuna mchezaji aliyefanikiwa kufunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja kama Aziz Ki. Wachezaji kama John Bocco, Simon Msuva, Meddie Kagere, na Amissi Tambwe wamewahi kutwaa kiatu cha dhahabu mara mbili ndani ya miaka 20 iliyopita.
Aziz Ki ameingia kwenye historia kwa kuwa kiungo pekee kufunga mabao mengi zaidi ndani ya msimu mmoja katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Rekodi hii ya kipekee inaashiria uwezo na kipaji chake cha hali ya juu katika uwanja wa mpira.
Leave a Comment