Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa anakaribisha maombi ya ajira kufuatia kibali kilichotolewa kwa mwaka wa ikama 2023/2024. Watanzania wenye sifa na uwezo wanahimizwa kutuma maombi kwa nafasi ifuatayo:
Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii Daraja la II – Nafasi 06
Majukumu ya Kazi
- Kuratibu shughuli za maendeleo ya jamii kwa kuzingatia jinsia.
- Kuhamasisha jamii kushiriki katika kupanga, kutekeleza, na kutathmini miradi yao ya maendeleo.
- Kutoa elimu kuhusu masuala ya kijinsia na kuondoa mila potofu.
- Kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi na matumizi yake.
- Kukusanya na kuchambua takwimu za kijamii kwa ajili ya kupanga mipango bora.
- Kuelimisha jamii kuhusu haki za watoto na umuhimu wa elimu ya watu wazima.
- Kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi kila mwezi.
- Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
Sifa za Mwombaji
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45.
- Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
- Awe amehitimu Astashahada/Cheti katika Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Sanaa kutoka taasisi inayotambuliwa na serikali.
Mshahara
Ngazi ya mshahara wa serikali – TGS B.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Kuambatanisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kuainisha ulemavu wao katika mfumo wa ajira.
- Kuambatisha wasifu binafsi (CV) yenye maelezo kamili pamoja na majina ya wadhamini watatu.
- Kuambatanisha nakala za vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria.
- Waombaji waliomaliza masomo nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE, TCU).
- Waombaji waliostaafu utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 05 Aprili 2025, saa 6:00 usiku.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao kupitia mfumo wa Ajira Recruitment Portal kwa anuani ifuatayo:
🔗 https://portal.ajira.go.tz
Maombi yote yaelekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA,
S.L.P 72, KYERWA.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatazingatiwa.
Leave a Comment