TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imepokea kibali cha ajira mpya kwa Kumb. Na. FA.228/613/01F/064 cha tarehe 13 Machi, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kwa mujibu wa kibali hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kwa nafasi ifuatayo:
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 1
1.1 Sifa za Mwombaji:
- Awe na elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.
- Awe na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.2 Kazi na Majukumu:
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
- Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu sahihi za huduma.
- Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za mkuu wa idara, na ratiba za kazi.
- Kupokea, kusambaza na kutunza majalada na nyaraka za ofisi.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.3 Mshahara:
- Ngazi ya mshahara ni TGS. C kwa mwezi kwa mujibu wa viwango vya Serikali.
MASHARTI YA JUMLA:
- Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu wao.
- Maombi yaambatanishwe na:
- Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Wasifu binafsi (CV) yenye anwani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini watatu.
- Nakala za vyeti vya taaluma na mafunzo mbalimbali vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliopata elimu nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na TCU/NACTE au NECTA.
- Barua ya maombi iliyoandikwa na kusainiwa na mwombaji.
- Waajiriwa wa Serikali waliopo kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
- Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utasababisha hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06 Aprili 2025.
Jinsi ya Kutuma Maombi:
- Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwa anwani: http://portal.ajira.go.tz.
- Maombi yoyote yatakayowasilishwa nje ya mfumo huo hayatafanyiwa kazi.
Anwani ya Mkurugenzi Mtendaji:
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI,
S.L.P 42,
SINGIDA.
Barua pepe: [email protected]
Tovuti: www.ikungidc.go.tz
Simu: +255262964037 / +255262964036
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI
Leave a Comment